MAJAMBAZI
sita akiwemo mwanamke mmoja, ambao majina yao hayajajulikana, Wameuawa
na Polisi jana majira ya saa usiku, katika tukio la kurushiana risasi
baina ya majambazi hayo na Askari Polisi eneo la Mlima Sekenke Wilaya ya
Iramba mkoa wa SIngida.
Majambazi
hayo yamedaiwa yalikuwa yamejipanga kwa lengo la kuteka magari kwenye
mlima huo wa Sekenke ili kupora mali za abiria na mizigo yao.
Mkuu
wa upelelezi mkoa wa Singida, Ayubu Tenge, alisema kuwa majambazi hayo
yamekamatwa yakiwa na bunduki aina ya SMG tatu na risasi 105 na mabomu
ya kutupa kwa mkono saba na moja walilotumia kuwarushia polisi.
Alisema taarifa kamili itatolewa na kamanda wa polisi mkoa wa Singida leo mchana, juu ya tukio hilo.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)