MABONDIA
wa ngumi za kulipwa Ramadhan Shauri na Bakari Dunda wataoneshana kazi
katika pambano lisili la ubingwa litakalofanyika Septemba 4 mwaka huu.
Pambano
hilo ambalo litakuwa la raundi nane litasindikizwa na burudani kutoka
katika kundi la 'Makhirikhiri wa bongo' huku likitanguliwa na mapambano
manne ya utangulizi ambapo yatafanyika katika ukumbi wa CCM Mwinjuma wa
Mwananyamala Dar es Salaam.
Akizungumza
Dar es Salaam jana, Mratibu wa pambano hilo Ibrahim Kamwe 'Bigright'
alisema maandalizi ya pambano hilo yamekamilika na kuwataka wadau wa
mchezo wa ngumi kuweza kujitokeza kwa wingi ili kushuhudia mapambano
hayo.
Bigright
aliyataja ambambano ya utangulizi ni kati ya Anthon Mathias na Shabani
Madilu ambapo pambano lao litakuwa la raundi sita.
Wengine
ni Joseph Mbowe na Ezekiel Ezekiel raundi nne, Isa Omari na Kade Hamis
raundi sita na Sadat Miyeyusho na Herman Richard raundi sita.
Pia
wamo Yona Miyeyusho na Haruna Said raundi nne, Martine Richard na
Jumanne Kilumbelumbe raundi nne na pambano la mwisho litakuwa kati ya
Mwaite Juma na Franck Pury raundi nne.
Mbali
na kuwepo mapambano ya ngumi kutakuwa na huzwaji wa DVD zenye mapambano
ya mabingwa wa Dunia akiwemo Manny Paquaio, Floyd Maywherth, Roy Jones
na wengine kibao.
DVD
hizo zilizoandaliwa kwa ubora wa hali ya juu zitakuwa zikiuzwa kwenye
mpambano huo na Kocha maarufu Rajabu Mhamila 'SUPER D BOXING COACH' hapo
na kwa Dar es Salaam DVD hizo zinapatikana katika Makutano ya Barabara ya Uhuru na Msimbazi
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)