Rostam Aziz katika moja ya mikutano yake ya Chama siku za nyuma. |
KADA wa Chama
Cha Mapinduzi CCM, Peter Kamfumu, ameongoza kura za maoni zilizopigwa
na Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Wilaya ya Igunga Mkoani Tabora kwa
ajili ya kuomba kugombea Ubunge Jimbo la Igunga lililoachwa wazi na
aliyekuwa Mbunge wa jimbo hilo, Rostam Azizi, aliyejiuzulu hivi
karibuni.
Taarifa
zilizopatikana kutoka mkoani Tabora zinaeleza kuwa, Kamfumu, ambaye pia
ni Kamishna wa Nishati katika Wizara ya Nishati na Madini, amepata kura
588 kati ya kura 928 zilizopigwa na Wajumbe wa Mkutano huo katika
uchaguzi uliofanyika jana Mjini Igunga.
Akizungumza
na Sufianimafoto kwa njia ya simu, Katibu wa CCM Wilaya ya Igunga,
Neema Adam, amesema kuwa katika kinyang'anyiro hicho walikuwa jumla ya
wagombea 13 wanachama wa CCM ambao wamepigiwa kura za maoni katika
mkutano huo na hatimaye Kamfumu kuibuka kidedea kwa kuongoza katika kura
hizo za maoni.
Aidha
aliwataja Wanachama wengine waliopigiwa kura kuwa ni pamoja na Jafari
Ali, aliyepata kura 163, Shamsi Feruzi, kura 36, Hamis Mapunda, kura
36, Ngasa Nikolaus kura 18, Seif Hamis, kura 13 na Shire Mashauri,
kura 16.
Wengine ni Hamad Safari, kura 5, Mkoba Shaban, kura 5, Daniel Mboje, kura 4, Adam Kamani, kura 3 na Amina Fundikila, kura 7.
Aidha
Katibu huyo wa CCM Wilaya ya Igunga alisema kuwa majina hayo yote
yatapelekwa ngazi ya Mkoa ambayo nayo itayapitia na kisha kuyapeleka
katika Kamati Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi kwa maamuzi zaidi.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)