BREAKING NEWS:BASI LA HOOD LAPATA AJALI MOROGORO WATU 4 WAFARIKI 29 MAJERUHI - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

BREAKING NEWS:BASI LA HOOD LAPATA AJALI MOROGORO WATU 4 WAFARIKI 29 MAJERUHI

Watu wanne wamedaiwa kufa papo hapo na wengine wawili kufia Hospital huku wengine zaidi ya 29 wakijeruhiwa vibaya baada ya basi la kampuni ya hood kupata ajali eneo ya Iyovi mpakani mwa mkoa wa Morogoro na Iringa.

kwa mujibu wa mtandao www.francisgodwin.blogspot.com umdepata kuwasiliana na mkuu wa kikosi cha usalama barabarani mkoa wa Morogoro (RTO)Lenard Gindo ambaye amedai kuwa pamoja na watu wawili kufa eneo la ajali watu wengine wawili walifariki baada ya kufika Hospital ya mkoa wa Morogoro.


RTO Gindo alisema kuwa ajali hiyo imehusisha basi la kampuni hiyo ya Hood lenye namba za usajili T 242 AAU ambalo lilikuwa likitoka Dar es Salaam kuelekea Tunduma mkoa wa Mbeya na kuwa ajali hiyo imetokea majira ya saa 6 mchana eneo la Msimba jirani na Iyovi mpakani mwa mkoa wa Morogoro na Iringa.

Alisema kuwa katika jali hiyo watu 29 akiwemo dereva wa basi hilo Issa Nyenza ndio ambao wamejeruhiwa na kuwa maiti moja kati ya 4 imepata kutambuliwa kwa jina moja la Yassin .

Hata hivyo alisema chanzo cha ajali hiyo na mwendo kasi na kupasuka kwa taili la mbele la basi hilo wakati likiwa katika mwendo mkali.
Habari kwa Hisani ya Francis Godwin

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages