Frank (kushoto) akiongea jambo Na Mh Naibu Spika Job Ngungai(katikati) akiwa na Mwenyekiti Wa Tanz Uk Dr John Lusingu
---
SALAAM,
---
SALAAM,
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Mheshimiwa
Job Ndungai , pamoja na shuguli nzito za kuongoza Ujumbe wa Wabunge
walioiwakilisha Taifa katika majadiliano ya BAE hapa Uingereza, alitumia
fursa ya siku ya mapumziko siku ya Jumapili na kufanya ziara fupi ili
kujifahamisha zaidi kuhusu shuguli za Diaspora hapa nchini
Uingereza. Akiwa mgeni wa Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Kitaifa, Dr John
Lusingu katika makazi yake mjini Reading, Mheshimiwa Ndungai , alipata
muda wa kufahamishwa jinsi ambavyo Jumuiya ya WaTanzania(TANZ-UK)
ilivyojipanga kushiriki katika mipango mbali mbali ya maendelo ya Taifa,
pamoja na kuwatumikia waTanzania waishio hapa Uingereza.
Mwenyekiti Jumuiya
hiyo kiTaifa, alimpongeza Mh Ndungai kwa kukubali kuongoza shuguli hiyo
ya mashauriano pamoja na changamoto zake. Dr Lusingu alisisitiza
kuwa chaguo la sector ya Elimu kama “mfaidi mlengwa” ni jambo la
kuungwa mkono na kila mTanzania baadala ya kuangalia kila jambo katika
mapungufu zaidi ya faida.
Dr Lusingu alimuahidi
Mh. Ndungai kuwa, kwa wakati muafaka, Jumuiya itawasiliana na vyombo
husika kuweza kuweka rasmi mkakati wa Jumuiya kujishirikisha na shuguli
za bunge. Kwa sasa Jumuiya isingependa kuchanganya mambo, ajenda kwa
sasa ni kuhakikisha kuwa lengo la ujumbe wake lifanikishwa kwanza. Mh.
Ndungai alifurahishwa na mikakati ya Diaspora ambayo aliita ya
kizalendo na yenye njozi zanazokubalika. Mh. Ndungai pia alifurahishwa
zaidi kusikia kuwa Diaspora ni mojawapo ya mafanikio ya serikali ya
awamu ya nne.
Mh. Ndungai
alikubaliana na kauli ya Dr John Lusingu, kuwa kwa wakati muafaka,
bunge nalo kwa kupitia vyombo husika vya serikali litajitahidi
kushirikiana na Diaspora katika maeneo mabali mbali ya ujenzi wa Taifa.
ASANTENI,
URBAN PULSE CREATIVE
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)