LUKAZA EXCLUSSIVE: WANAFUNZI UDOM WAANZA KURUDISHWA KWA MAKUNDI, KUNDI LA KWANZA NI MWAKA WA 3 - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

LUKAZA EXCLUSSIVE: WANAFUNZI UDOM WAANZA KURUDISHWA KWA MAKUNDI, KUNDI LA KWANZA NI MWAKA WA 3

 Wanafunzi Wa Mwaka Wa 3 Wa Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM) wakiwa katika Makundi Mara baada ya kuwasili eneo la usahili katika kiwanja cha Mpira kilichopo Karibu na Idara ya Maji Safi na Maji Taka (DUWASA) Na Zinapojengwa Ofisi Za Benki Kuu Dodoma Mchana Huu
Wanafunzi Wa Mwaka Wa 3 UDOM wakiwa katika mistari wakiendelea na Usajili Mchana Huu Katika Kiwanja Cha Mpira kilichopo Karibu na Idara ya Maji Safi na Maji Taka (DUWASA)
Wazee Wa Kufanya Massage (FFU) wakiwa Katika Eneo La Tukio Wakilinda Usalama Kwa Kudhani Wanafunzi Wanaweza Kuanzisha Tena Mgomo Ambao Ulipelekea Kufungwa Kwa Chuo Kwa MUda Usiojulikana Na Kupelekea Wanafunzi Kuanza kurudishwa Kwa Makundi Na Kundi la Kwanza Ni hili La Mwaka Wa 3 Ambao Wanafanyiwa Udahili Upya Mchana Huu
Wanafunzi wa Mwaka Wa 3 na Kundi la Kwanza Kurudishwa kwa Mafungu Wakiwa katika Foleni Kabla Ya Kuanza Kufanyiwa Udahili Upya Mchana Huu katika Kiwanja Cha Mpira Kilichopo Mita 200 Kutoka Idara ya Maji Safi Na Maji Taka Dodoma (DUWASA).
...................................
Kutokana Na Mgomo Uliotokea UDOM tarehe 13 JUNE hadi 15 June 2011 Na Kupelekea Kitivo Cha Sayansi Ya Jamii Sanaa na Lugha Cha Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM) Kufungwa Kwa Muda Usiojulikana Hatimaye Wanafunzi Wameanza Kurudishwa Kwa Mafungu Na Fungu la Kwanza ni La Wanafunzi Wa Mwaka Wa 3 ambao Leo wanaendelea Na Udahili na udahili huo utaendelea hadi kesho jumapili na Jumatatu Wataanza Mitihani Yao Ya Kumaliza Miaka Yao Mitatu Chuoni Hapo

Mgomo Huo Ulitokana Na Wanafunzi Kudai Field Na Kusababisha Kitivo Cha Sayansi Ya Jamii, Sanaa na Lugha Cha UDOM Kufungwa Kwa Muda usiojulikana Na Hatimaye Leo Wanafunzi Wameanza Kurudishwa Kwa Mafungu Baada ya Kukaa Nyumbani Wiki Mbili tokea Chuo Kilipofungwa Kwa Muda usiojulikana.

Makundi Mengine Ni Ya Mwaka Wa Pili Na Wa Kwanza Ambao Mpaka Sasa Haijulikani Ni Lini Makundi Haya Yatarudishwa Kufanya Mitihani yao ya Kumaliza Mwaka Wa Masomo na Kuweza kuingia Kwa Mwaka Mpya Wa Masomo.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages