Mkurugenzi
Mkuu Mtendaji wa Hospitali ya CCBRT , Erwin Telemans, akiagana na
mjumbe wa bodi ya udhamini wa mfuko wa huduma kwa jamii wa kampuni ya
simu za mkononi ya Vodafone ya nchini Uingereza, Elizabeth Filkin, baada
ya kumaliza ziara yake hospitalini hapo leo mchana (wapili kulia) ni
Ofisa Mkuu wa Masoko na Uhusiano wa kampuni hiyo, Mwamvita Makamba,
aliembatana na ujumbe huo na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali
hiyo, Haika Mawalla.
Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya CCBRT Bw
Erwin Telemans akimpatia maelezo Mjumbewa Bodi ya Udhamini wa Mfuko wa
Huduma kwa Jamii wa Vodafone ya nchini Uingereza, Elizabeth Filkin,
wakiwa katika wodi ya wagonjwa wa mdomo sungura alipotembelea
hospitalini hapo kuona maendeleo ya miradi inayofadhiliwa na Vodacom
Foundation. Kushoto ni Ofisa Mkuu wa Masoko na Uhusiano wa Vodacom
Tanzania Mwamvita Makamba, akimjulia hali mtoto mwenye
tatizo la mdomo sungura. Elizabeth yupo nchini kwa ajili ya kukagua
miradi mbalimbali ya kijamii inayofadhiliwa na Vodacom.
Mjumbe
wa bodi ya udhamini wa mfuko wa huduma kwa jamii wa kampuni ya simu za
mkononi ya Vodafone ya nchini Uingereza Elizabeth Filkin akipewa maelezo
na mwenyeji wake Mkurugenzi Mkuu Mtendaji wa Hospitali ya CCBRT Bw.
Erwin Telemans kuhusiana na wagonjwa wanaopata huduma katika Hospitali ya CCBRT ya jijini Dar es Salaam.
Muuguzi wa Hospital ya CCBRT kitengo cha wagonjwa wa Fistula Bi. Emelda
Lweno akimwonyesha mjumbe wa bodi ya udhamini wa mfuko wa huduma kwa
jamii wa kampuni ya simu za mkononi ya Vodafone ya nchini Uingereza Elizabeth Filkin wanawake wenye ugonjwa wa Fistula ambao matibabu yake yanafadhiliwa na Kampuni ya Vodacom Tanzania wakati wa ziara yake hospitalini hapo.
Muuguzi wa Hospital wa Hospitali ya CCBRT kitengo cha wagonjwa wa Fistula, Emelda Lweno akitoa maelezo kuhusiana na jinsi wanavyowahudumia wagonjwa wa Fistula.
Mkurugenzi
Mkuu Mtendaji wa Hospitali ya CCBRT Bw. Erwin Telemans akifafanua jambo
kwa mjumbe wa bodi ya udhamini wa mfuko wa huduma kwa jamii wa kampuni
ya simu za mkononi ya Vodafone ya nchini Uingereza Elizabeth Filkin.Picha Na Muhidin Sufian
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)