Waziri
Mkuu wa zamani,Edward Lowassa(Kushot0)akimkabidhi Bahasha yenye Tsh.
milioni 13, Mufti wa Tanzania, Sheikh Mkuu,Issa Shaaban bin Simba,kwa
ajili ya kusaidia shule ya sekondari la Edward Lowassa iliyopo
Kigamboni,Dar es Salaam.Kwa mujibu wa Mufti ambaye ni mlezi wa shule
hiyo, Shule hiyo inatarajiwa kufunguliwa rasmi mwakani kwa kuanzia na
wanafunzi 200 wa kidato cha kwanza, na kwamba fedha hizo zitatumika
kukamilisha baadhi ya mambo ya shule hiyo ikiwemo kujenga bweni la
watoto 30, choo cha shule, kisima cha maji na shule itajihusisha zaidi
kusomesha yatima na watoto wanaoishi katika mazingira magumu. Kulia ni
aliyekuwa Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam,Alfred
Tibaigana ambaye pia ni mlezi wa shule hiyo.
Edward
Lowassa(kulia)akimsindikiza Mufti wakati akiondoka baada ya hafla ya
kumkabidhi fedha hizo,iliyofanyika Ofisini kwake,Mikocheni, Dar es
Salaam.
Wakiagana baada ya shughuli hiyo.Picha na Mdau Bashir Nkromo
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)