Mwenyekiti
wa chama cha Wanamuziki,Tanzania Flava Unit akizungumza mapema leo
kuhusiana na uzinduzi wa video ya miaka 50 ya uhuru wa sanaa ya
Muziki,video hiyo imefanywa na kampuni ya Visual Lab,ina jumla ya dakika
zisizozidi nne ili watazamaji wasichoke, na ina wasanii zaidi ya 50
huku walioingiza sauti wakiwa 36. Watayarishaji wa Audio ni Marco Challi
na Lamar, wakati video imefanywa na Adam Juma wa Visual Lab.
Msemaji
Mkuu wa Tanzania Flava Unit,Mkubwa Fella akiwatambulisha viongozi
waandamini wa chama hicho,mapema leo kwenye viwanja vya Lidaz
Club,Kinondoni jijini Dar.kushoto kabisa ni Mjumbe wa chama hicho
Keisha.
Msemaji
mkuuu wa chama cha Tanzania Flava Unit,Mkubwa Said Fella akiendelea
kuwatambulisha viongozi wa chama hicho,shoto kabisa ni Mjumbe Banana
Zorro,Prodyuza wa Chama hicho Lamar Niekamp kutoka Fish Crub,Katibu
Kalla Pina na anaefuata kushoto ni Khalid Mohamed ambaye ni Mwenyekiti
Msaidizi wa Tanzania Flava Unit.
Baadhi
ya Waandishi wa habari pamoja na wadau wengeine wakiangalia 'DEMO' ya
video hiyo iliyozinduliwa leo kwenye viwanja vya Lidaz Club,Kinondoni
jijini Dar.
Ndugu zangu habari za mchana,
Nachukua
fursa hii kuwakaribisha katika uzinduzi wa video ya wasanii
inayohusiana na sherehe za miaka 50 tya uhuru wa Tanzania, hii ni sehemu
yetu na sisi ya kusherehekea kama vijana tukionesha kuguswa kwetu na
hili, na wakati huo huo tukijaribu kuonesha mchango wetu kama vijana kwa
serikali yetu ambayo kwa njia moja ama nyingine inahitaji shukrani,
kwani ndiyo iliyotufikisha hapa tulipo.
Tuna
uhuru, tuna amani na mambo yanaenda ingawa matatizo ya hapa na pale
yapo, lakini tumeangalia upande mzuri zaidi na tumeona kabisa huu ndio
muda muafaka wa kukumbushana pale tuilipojikwaa, ili tupate kwernda kwa
mwendo mzuri.
Katika
miaka hii 50 ya Uhuru sanaa ya muziki ni moja kati ya sekta ambazo
zimeleta ajira kwa vijana. Unaweza kuona jinsi wasanii mbali mbali
walivyojikwamua kupitia muziki, mifano hai imo hata humu ndani, watu
wanaendesha magari, watu wanaishi kwenye nyumba nzuri na wana miradi yao
kupitia muziki huu wa kizazi kipya.
Si
vibaya basi kwa kile kidogo unachokipata kukitolea shukrani, kuonesha
kwamba unakithamini, sisi twajivunia miaka 50 ya uhuru na tunahisi
kwamba tuna kila haja ya kusherehekea.
Sisi
kama Tanzania Flava Unit, vijana ambao tuko katika sekta ya muziki
tuliojikusanya kwa lengo la kuufikisha muziki wetu katika eneo jingine
kimaudhui tumepania kufanya matamasha mengi tu nchi nzima, katika
kusherehekea hili na yote haya yatakuwa ya wazi, na tutakuwa tukitoa
burudani kwa watanzania, tukisherehekea nao pamoja miaka hii 50.
Kwa
fikra zetu hii ni muhimu, kuna wakati mtanzania anahitaji burudani na
hawezi kuingia sehemu kulipa wala hawezi kufika mahali mbali kabisa
akaniona ama mimi, au Chegge ama temba, kwa nini tusimfikie na kumpa
burudani?
Hilo lilikuwa wazo la kwanza.
Lakini
jingine ni kwamba kuna wakati mtanzania anahitaji kuburudika,
kashafikiria sana mfumuko wa bei, kafikiria sana suala la umeme ambalo
linatusumbua wengi na kafikiria sana ugumu wa maisha, na mwisho wa siku
akitoka nje katika uwanja wa karibu anapata burudani angalau
anachangamsha ubongo wake na kuanza kujua kesho atakabiliana vipi na
ugumu huu wa maisha ambao kila kukicha tunajitahidi kuhakikisha kwamba
tufike sehemu, ila mtu apate unafuu.
Tuko katika hatua za mwisho kabisa kupata udhamini wa kufanya matamasha haya, na tukiwa tayari tutawafahamisha.
Video
hii imefanywa na kampuni ya Visual Lab, ina jumla ya Dakika zisizozidi
nne ili msichoke, na ina wasanii zaidi ya 50 huku walioingiza sauti
wakiwa 36.
Watayarishaji wa Audio ni Marco Challi na Lamar, wakati video imefanywa na Adam Juma wa Visual Lab.
Hili ndio kubwa kwa leo kaka na dada zangu iwapo kuna la ziada tutaambiana!
Hamis Mwinjuma.
Mkurugenzi
Tanzania Flava Unit










No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)