Waziri wa Nishati na Madini William Ngeleja (katikati)
akijadiliana na Mbunge wa Jimbo la Sumve Richard Ndassa (kulia) na
Kushoto ni Waziri wa Uwekezaji na Uwezeshaji, Dk. Mary Nagu ambaye pia
ni Mbunge wa Jimbo la Anan leo mjini Dodoma.
Waziri wa Nishati na Madini
William Ngeleja akijadiliana jambo na baadhi wa wabunge mara baada ya
kuwasilisha hotuba yake ya Makadirio ya Matiumizi ya Fedha za wizara
hiyo kwa mwaka 2011/2012 Bungeni leo mjini Dodoma.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge
ya Nishati na Madini,Januari Makamba(Kulia)akizungumza jambo na
kusalimiana na Mbunge wa Jimbo la Lushoto Henry Shekifu mara baada ya
kuwasilisha taarifa ya kamati hiyo kuhusu utekelezaji wa majukumu ya
wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2010/2011 pamoja na makadirio ya
mapato na matumizi ya wizara hiyo kwa mwaka 2011/2012 bungeni leo
mjini Dodoma.
Picha na Magreth-MAELEZO





No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)