|
|
|||||
Youths of United Nations Association of Tanzania
7th
July, 2011
Taarifa
kwa Vyombo Vya Hahabri
Asasi
ya Vijana wa Umoja wa Mataifa Tanzania (YUNA TZ) kwa kushirikiana na United Nations
Alliance of Civilizaation (ambao pia ni wadhamini wakuu wa mradi huu),
wanatekeleza mradi wa Ushiriki na Ushirikishwaji wa Vijana katika Kuendeleza
Amana, Usalama na Haki za Binadamu nchini Tanzania.
Mradi
huu, Unatekelezwa katika mikoa kumi (10) ya Tanzania ambayo ni Mwanza, Dodoma,
Mtwara, Kigoma, Mbeya, Ruvuma, Zanzibar, Tanga, Arusha and Dar es Salaam. Mradi
huu ambao umeanza kutelezwa tangu mwishoni mwa 2010, una ngazi kuu mbili za
utekelezaji ambapo, ngazi ya kwanza ilihusisha kubaini vijana ishirini (20) kuwa
Vijana wawezeshaji wa kitaifa. Vijana wawezeshaji hao walijengewa uwezo katika
maeneo husika ya mradi ili waweze kuwafundisha vijana wengine pia. Katika ngazi
ya pili, Vijana wawezeshaji wataenda katika mikoa yote 10 ya Tanzania na
kuwafundisha vijana wenzao.
Malengo
makuu ya mradi huu wa Ushiriki na Ushirikishwaji wa Vijana katika kuendeleza
Amani, Usalama na Haki za Binadamu ni kama ifuatavyo;-
·
Kuwajengea
uwezo vijana ili waweze kushiriki ipasavyo katika kuimarisha na kuendeleza
Amani, Usalama na kulinda na kutetea Haki za Binadamu.
- Kujenga na kuendeleza utamaduni wa kuheshimiana na kuvumiliana katika mitizamo na Nyanja mbalimbali za kisiasa, kiutamaduni na kidini pamoja na kukuza uwajibikaji kwa kila mtu.
- Kusadia na kuendeleza jukwaa la majadilino baina ya kundi rika la vijana na makundi rika mengine ili kukuza ushirikiano na kuendeleza majadiliano ya masuala muhimu ya ustawi wa Taifa letu bila kusababisha madhara hasi na pasipo kugombana.
Asasi
ya Vijana ya Umoja wa Umoja wa mataifa inapenda kuutangazia umma wa wa-Tanzania
na wadau wote wapenda Amani na Maendeleo kuhusu mradi huu muhimu ili kwa pamoja
tuweze kuilinda Tanzania yetu iendelee kustawi zaidi na kuwa mahala salama na
pazuri pa kuishi kwa ajili ya kizazi cha leo na cha baadae.
Mungu Ibariki
Tanzania
Lawrence E.
Chuma
Mratibu





No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)