YAH: TAMKO LA PPAT KULAANI KUSHAMBULIWA KWA MPIGAPICHA HERI SHABANI WA GAZETI LA MAJIRA NA MWANDISHI CHRISTOPHER LISA WA SANI.
Chama
cha Wapigapicha za Habari Tanzania (PPAT) kinapenda kuungana na
watanzania wote kulaani kitendo cha Kinyama alichofanyiwa Mpigapicha wa
Gazeti la Majira na Mwandishi wa Sani, kwa kuvamiwa na wananchi,
kupigwa na kuporwa mali zao wakati wakiwa kazini kuripoti tukio la
vurugu za kundi la vijana waliokuwa wakishambulia polisi kwa mawe baada
ya Polisi kuchukua Mwili wa Marehemu Bakari Hamisi ambaye ndugu zake
waligoma kuu zika Julai 6, 2011 huko Manzese Dar es Salaam.
Kitendo walicho fanyiwa Wanahabari hao ni cha Kinyama na katu hakiwezi kuvu milika.
Hivyo
tunaliomba Jeshi la Polisi lifanye kazi yake ipasavyo na kuhakikisha
wote waliofanya vurugu hizo wanapatikana na kufunguliwa mashitaka kwa
vitendo hivyo vya vurugu na kujeruhi watu na kuharibu mali.
Kumekuwapo
na vitendo vingi vya kinyama wanavyofanyiwa Waandishi wa Habarui hasa
Wapigapicha kwa kupigwa na wananchi ama Polisi ambao kimsingi wanajua
kazi na wajibu wa Wanahabari katika jamii.
Pia
hivi karibuni, katika Maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya Sabasaba
yanayoendelea Mpigapicha wa Mwananchi Communication Fidelis Felix akiwa
kazini alishambuliwa na kuharibiwa Camera yake na Askari.
PPAT
inapenda kuliomba Jeshi la Polisi kutoa elimu kwa Askari wake kuwa
Mwandishi wa Habari si mtu wa kubugudhiwa na kupigwa wakati wanafanya
kazi zao kwani kufanya hivyo ni kuinyima haki jamii kupata habari
mbalimbali zinazo tokea katika jamii.
PPAT inawapa pole Heri Shabani na Christopher Lissa kwa mswaibu yaliyowafika na Mungu awape nguvu na kurejea tena katika kazi.
Mwasiliano zaidi
0717002303/0755 373999
0717002303/0755 373999
Mroki Mroki
Katibu Mtendaji PPAT.
Katibu Mtendaji PPAT.






No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)