Naibu
Waziri wa Utamaduni kutoka nchini China, Zhao Shaohua, akiangalia
zawadi ya picha ya pundamilia aliyopewa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinga
(kushoto) wakati naibu waziri huyo alipomtembelea ofisini kwake mjini
Dodoma jana.
Zhao pamoja na ujumbe wake wako nchini kwa ziara ya kikazi ya siku nne ikiwa na malengo ya kuimarisha mahusiano ya kitamaduni baina ya Tanzania na China.
Waziri Mkuu,Mizengo Pinga, akiangalia zawadi ya chombo cha kuwekea sukari alichopewa na Naibu waziri wa Utamaduni wa China, Zhao Shaohua (kulia) wakati naibu waziri huyo alipomtembelea ofisini kwake mjini Dodoma jana.
Mkurugenzi
Msaidizi wa Maendeleo ya Utamaduni, Anjela Ngovi, akimvalisha kanga
Naibu Waziri wa Utamaduni wa China, Zhao Shaohua, wakati naibu waziri
huyo alipotembelea mjini Dodoma jana kwa ajili ya kuonana na viongozi wa
Serikali huku waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Emmanuel Nchimbi (katikati) na Mkurugenzi wa Idara ya Utamaduni Prof. Helmasi Mwansoko (kulia) wakishuhudia .
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na
Michezo, Emmanuel Nchimbi (kulia) akisalimiana na Naibu Waziri wa
Utamaduni wa China, Zhao Shaohua (katikati) baada ya kuwasili kwenye
uwanja wa ndege wa mjini Dodoma leo Kulia ni Zhao Haisheng aliyeapambana na ujumbe huo.
Picha na Anna Nkinda - Maelezo
Naibu
waziri wa Utamaduni wa China, Zhao Shaohua, akiangalia ngoma ya kabila
la kisukuma iliyokuwa inachezwa na kikundi cha ngoma cha Mwinamila cha
mjini Dodoma baada ya Naibu Waziri huyo kuwasili mjini Dodoma jana.Picha zote na Anna Nkinda-MAELEZO
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)