YALIYOJIRI BUNGENI DODOMA JUZI, WENJE ATOLEWA NJE, WABUNGE WASUTANA NJE YA BUNGE NUSURA KUCHOMANA VIDOLE VYA MACHO - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

YALIYOJIRI BUNGENI DODOMA JUZI, WENJE ATOLEWA NJE, WABUNGE WASUTANA NJE YA BUNGE NUSURA KUCHOMANA VIDOLE VYA MACHO

Mbunge wa Nyamagana (CHADEMA) Ezekia Wenje (aliyevaa suti ya rangi ya maziwa) akitolewa nje ya ukumbi wa Bunge na Askari Polisi wa Bunge baada ya kutomtii Mwenyekiti wa kikao cha Bunge cha leo Mbunge wa Dole (CCM) Silvester Mabumba, alimtaka kukaa chini na kutokutoa hoja ya dharula kuhusu Samaki wa sumu kutoka Japan.
Mbunge wa Nyamagana (CHADEMA) Ezekia Wenje (aliyevaa suti ya rangi ya maziwa) akitolewa nje ya ukumbi wa Bunge na Askari Polisi wa Bunge.
Baadhi ya mawaziri wakimpongea waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika Prof. Jummanne Maghembe mara baada ya Bunge kupitisha Bajeti ya wizara yake jana jioni katika kikao cha Bunge la bajeti kinachoendelea mjini Dodoma.

NJE YA UKUMBI WA BUNGE
Mbunge wa Ludewa (CCM) Deo Filikunjombe (kushoto) akisutwa nje ya ukumbi wa Bunge na Mbunge wa viti Maalum (CHADEMA) Suzan Kiwanga (aliyevaa kitenge) baada ya Filikunjombe kumwambia, Ezekia Wenje, mbunge wa Nyamagana (CHADEMA) (hayupo pichani) alikosa ustaarabu kwa kutokumtii Mwenyekiti wa kikao cha Bunge cha leo Mbunge wa Dole (CCM) Silvester Mabumba pale alipomwambia akae chini na kutokutoa hoja ya dharula kuhusu Samaki wa sumu kutoka Japan.
Mbunge wa Ludewa (CCM) Deo Filikunjombe (kulia) akisutwa nje ya ukumbi wa Bunge na wabunge wa viti Maalum (CHADEMA) Philipa Mturano (kushoto) Suzan Kiwanga (aliyevaa kitenge) na Mbunge wa jimbo la Kasulu mjini (NCCR – MAGEUZI) Moses Machari.
Mbunge wa Ludewa (CCM) Deo Filikunjombe (kushoto) akisutwa nje ya ukumbi wa Bunge na baadhi ya wabunge wa upinzani Moses Machari (kulia), Philipa Mturano (katikati) na Ezekia Wenje (kushoto) baada ya Filikunjombe kumwambia Wenje kuwa alikosa ustaarabu kwa kutokumtii Mwenyekiti wa kikao cha Bunge cha leo Mbunge wa Dole (CCM) Silvester Mabumba pale alipomwambia akae chini na kutokutoa hoja ya dharula kuhusu samaki wa sumu kutoka Japan.
Mbunge wa Ludewa (CCM) Deo Filikunjombe (kulia) akisutwa nje ya ukumbi wa Bunge na wabunge wa viti maalum (CHADEMA) Philipa Mturano (kushoto ) na Maryam Msabaha (katikati). Picha Zote na Anna Nkinda-MAELEZO

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages