MAHAKAMA YA KISUTU 'YAMTEMA' MMOJA WA KESI YA RICHMOND - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

MAHAKAMA YA KISUTU 'YAMTEMA' MMOJA WA KESI YA RICHMOND

Gire akiwa na uso wa furaha wakati akitoka kwenye Mahakama ya Hakimu  Mkazi Kisutu baada ya kuachiwa huru jana.

MAHAKAMA  ya Hakimu Mkazi Kisutu  ya jijini Dar es Salaam, imemwachia huru, Naeem Gire,  aliyekuwa anakabiliwa na kesi ya kughushi na kuidanganya Serikali kuwa mitambo ya kuzalisha umeme ya ‘Richmond’  ina uwezo wa kufua megawati 100 za umeme.

Baada ya kuachiwa huru mshitakiwa huyo, Gire,  alitoka kizimbani akichekelea baada ya hakimu wa mahakama hiyo, Waliarwande Lema , kutamka kuwa anamuona mshitakiwa huyo kuwa hana  kesi ya kujibu kutokana na ushahidi uliotolewa na upande wa Serikali uliofikishwa mahakamani hapo  kushindwa kukidhi vigezo vya kumtia hatiani.

“Baada ya kupitia ushahidi katika vipengele vyote,  nimeona kuwa hakuna ushahidi wa kutosha uliowasilishwa  ukionyesha kuwa mshitakiwa ana hatia na kuwa na  kesi ya kujibu,

Kesi hii ni miongoni mwa kesi kadhaa ambazo huletwa mahakamani na kisha kuitwisha lawama mahakama", alisema Hakimu  Mkazi wa Mahakama hiyo, Waliarwande Lema.Picha Na Sufiani Mafoto.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages