BMP
inayoandaa mashindano ya Redds Miss Temeke leo imetangaza zawadi kwa
washindi wa shindano hilo, ambapo awali wa kampuni hiyo, Benny Kisaka
aliwashukuru wadhamini wake wakuu kampuni ya Bia ya TBL kupitia kinywaji
chake cha Redds Original sanjari na Vodacom Tanzania kampuni
inayoongoza kati ya kampuni za simu za mkononi nchini ambao pia ni
wadhamini wakuu wa Miss Tanzania ambako washindi watatu wa Jumamosi
watakwenda kushiriki mashindano hayo mwaka huu.
Pia
gazeti la Jambo Leo, Saluni ya kisasa iliyopo katikati ya Jiji ya
Sally, 88.4 Clouds FM Redio ya watu, Office Direct, 100.5 Times FM,
Jambo Tours na Fredito Entertainment.
Katika
zawadi hizo ambazo mshindi atamrithi Genevevive Mpangala, ukiondoa
zawadi ya kifuta jasho, maeneo mengine yote yameboreshwa ukilinganisha
na mwaka jana kwa taji la Temeke Jumamosi, ambapo mwaka jana kifuta
jasho kilikuwa ni Sh 200,000 kila mmoja na kinabaki hivyo.
Nyongeza
ipo kwa mshindi wa nne na tano kwa kuwa wanaingia katika ya fainali ya
Redds Miss Temeke mwaka jana mshindi wa nne alipata Sh 300,000 na wa
tano alinyakulia Sh 400,000.
Mwaka
huu kutokana na udhamini wa kiwango cha juu kutoka TBL na Vodacom pia,
washindi hao wa nne na tano kila mmoja atapata Sh. 500,000. Mshindi wa
tatu mwaka jana alipata Sh.800,000 Jumamosi Julai 16 mwaka huu atapata
Sh milioni 1.
Zawadi
pia imeongezwa kwa mshindi wa pili ambaye mwaka jana alipata Sh milioni
1.2 na sasa atapata Sh milioni 1.5 likiwa ongezeko la shilingi laki
tatu. Kwa mshindi kwanza ambayo mwaka jana ilikuwa milioni 1.5, mwaka
huu Redds Miss Temeke 2011, atazawadiwa kitita cha Shilingi milioni 2
taslim
Wenzetu
wa Vodacom wamekuja na mpango kabambe wa kutoa zawadi hizo za pesa
kupitia mtandao wa M-Pesa papo hapo ukumbini na watakuwa na mtaalamu wao
kuhakikisha zoezi hilo linafanyika katika matarijio yasiyo tatu ili
stahiki ya kila mshiriki ipatikane kwa wakati huo.
Shindano
hilo lilinogeshwa na kundi la B-Band linaloongozwa na mwanamuziki
Banana Zorro, sanjari na baba yake mzazi, Zahir Ally na msanii AT kutoka
Zanzibar ambaye ni mtunzi wa nyimbo za Nipigie, Mama Ntilie, Samaki na
sasa Vifuu Tundu.
Warembo
wengine waliopata kutwaa taji la Miss Temeke na miaka yao kwenye mabano
ni Asela Magaka (1996), Miriam Odemba (1997), Ediltruda Kalikawe
(1999), Irene Kiwia (2000), Happiness Magasse (2001), Regina Mosha
(2002), Sylvia Bahame (2002) na Cecylia Assey (2004).
Wengine
ni Jokate Mwegelo (2006), Queen David (2007) na Angela Lubala (2008),
Sia Ndaskoi (2009) na Vodacom Miss Tanzania wa sasa, Geneveive Mpangala.
Picha Na Full Shangwe Blogu
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)