RICHA ADHIA KUWANOA WALIMBWENDE WA REDDS MISS KINONDONI - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

RICHA ADHIA KUWANOA WALIMBWENDE WA REDDS MISS KINONDONI


 Richa Adhia
----
WAREMBO wanaotarajiwa kuwania shindano la kumsaka Redd’s Miss Kinondoni wanatarajiwa kuingia kambini keshi katika hoteli ya Giraffe Ocean View.

Mkurugenzi wa Boy George Promotions inayoandaa shindano hilo, Rahma George amewataja warembo hao kuwa ni pamoja na  Fatma Pongwa, Winnie Gerald, Mariam Almas, Stellah Premsing, Hamisa Hassan,StellaMbuge, HUsna MAulid, Felister Philip, Stella Morris, Naomi Jones, Pamela Gordian, Renalda Apojei na Sabrina Abdallah.

Rahma alisema warembo hao watakuwa wakinolewa na Miss Tanzania mwaka 2007, Richa Adhia ambapo shindano limepangwa kufanyika Julai 23 katika ukumbi wa Mlimani City, jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages