Mkazi wa Pongwe Tanga, Zainabu Hamza (kulia) akipewa ushauri nasaha kuhusu ugonjwa wa ukimwi mara baada ya kupima damu wakati wa uzinduzi wa kampeni ya uhamasishaji kuhusu ugonjwa wa HIV/AIDS
iliyoandaliwa na kampuni ya Saruji Tanga katika mji wa Pongwe mkoani humo jana. Anayetoa ushauri ni muuguzi kutoka katika Hospitali ya Mkoa ya Bombo, Elizabeth Lawuo. Anayeangalia ni mtoto wa Selina, Amina Adamu.
iliyoandaliwa na kampuni ya Saruji Tanga katika mji wa Pongwe mkoani humo jana. Anayetoa ushauri ni muuguzi kutoka katika Hospitali ya Mkoa ya Bombo, Elizabeth Lawuo. Anayeangalia ni mtoto wa Selina, Amina Adamu.
Mkazi wa Pongwe Tanga, Hadija Rashidi (kulia) akipima virusi vya ukimwi wakati wa uzinduzi wa kampeni ya uhamasishaji kuhusu ugonjwa wa HIV/AIDS iliyoandaliwa na kampuni ya Saruji Tanga katika mji wa Pongwe mkoani humo jana. Anayemtoa damu ni muuguzi kutoka katika Hospitali ya Mkoa ya Bombo, Immaculata Kadaga.
Mkazi wa Pongwe Tanga, Selina Anthony (kulia) akipima virusi vya ukimwi wakati wa uzinduzi wa kampeni ya uhamasishaji kuhusu ugonjwa wa HIV/AIDS iliyoandaliwa na kampuni ya Saruji Tanga katika mji wa Pongwe mkoani humo jana. Anayemtoa damu ni muuguzi kutoka katika Hospitali ya Mkoa ya Bombo, Immaculata Kadaga na mtoto aliyebebwa ba Selina ni mjukuu wake, Gerald Rashidi.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Saruji Tanga, David Lee (kulia) akitolewa damu kupima virusi vya ukimwi wakati wa uzinduzi wa kampeni ya uhamasishaji kuhusu ugonjwa wa HIV/AIDS iliyoandaliwa na kampuni hiyo kwa wakazi wa mji wa Pongwe mkoani humo jana. Anayemtoa damu ni muuguzi kutoka katika Hospitali ya Mkoa ya Bombo, Immaculata Kadaga.
NA MWANDISHI WETU
Pongwe Tanga.
KAMPUNI ya Saruji Tanga
imezindua kampueni ya siku nne kuhusu masuala ya ufahamu juu ya ugonjwa wa
HIV/AIDS na upimaji wa virusi vya ugonjwa huo katika kata ya Pongwe mkoani
Tanga jana ikiwa ni sehemu ya sera za kampuni hiyo katika kuisaidia jamii (CSI).
Akizungumza wakati wa
uzinduzi huo Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Tanga Cement, David Lee alisema Tanga
Cement imeona kuna umuhimu mkubwa wa kufanya kampeni hiyo kwani maendeleo ya
Taifa lolote yanatokana na kuwa na watu wenye afya bora.
“Tanga Cement inajenga
Tanzania, hivyo tunaamini kuwa huwezi kujenga Taifa kama wananchi wengi
watakuwa hawana afya hususani vijana ambao ndio nguvu kazi kubwa katika uchumi
wan chi hii”, akasema.
Mkurugenzi huyo alisema
kampeni kama hiyo ilianzia kwanza kwa wafanyakazi wao pamoja na familia zao
katika mkakati huo huo kwamba ugonjwa wa ukimwi unazorotesha afya hivyo kampuni
haitaweza kutimiza malengo yake endapo idadi kubwa ya wafanyakazi watakuwa ni
waathirika.
“kama ilivyo kauli mbiu
yetu katika kampeni hii kuwa ’Okoa Maisha Pima Afya yako’ hivyo tunaamini
ukijua hali yako ukiwa umeathirika au hujaathirika itakusaidia kujiokoa wewe,
familia yako na wale wanaokuzunguuka”, akaongeza.
Akizungumzia
utekelezaji wa zoezi hilo, Ofisa Mawasiliano wa TCCL, Bi. Mtanga Noor alisema
wanatarajia kuhudumia zaidi ya wakazi 600 katika eneo hilo la Pongwe na kijiji
cha Kichangani vyote vikilizunguuka eneo ya kiwanda na makazi ya wafanyakazi wa
kampuni hiyo.
“Hawa majirani zetu
hivyo afya zao ni muhimu pia na ndio sababu moja ya vipengele tunavyoangalia
katika mpango wetu wa kuisaidia jamii (CSI) ni afya, na ukimwi unaingia katika
kipengele hiki”, akasema.
Bi. Mtanga akasema
katika kampeni hiyo ya siku nne wananchi hao watapata ushauri nasihi kuhusu
ugonjwa huo, kuchunguzwa afya zao ambapo zaidi ya shs milioni 17 zitatumika
kufanikisha zoezi hilo.
Awali akizungumzia hali
ya ugonjwa huo Mratibu Ukimwa mkoani humo, Moses Kisibo aliishukuru Tanga Cement
kwa kufanikisha zoezi hilo litakalosaidia kupunguza kasi ya maambukizi katika Mkoa wa Tanga akisema kuwa
kwa sasa ipo zaidi ya aslimia 8.7
Mratibu huyo alitaja
moja ya sababu inayochangia kuongezeka kwa kasi ua ugonjwa huo kuwa ni uelewa
mdogo kuhusu HIV/AIDS kwa wakazi wa mkoa huo ambapo zaidi ya asilimia 75 ya
watu wanaojijihusisha na masuala ya ngono wanafanya ngono za gizani.
“Kondomu hazitumiki
watu wanafanya ngono ‘gizani’ na hata hao wanaozitumia hawazitumiii jinsi
inavyotakiwa kwa kufuata hatua zinazoshauriwa na wataalamu hii inachangia kasi
ya ugonjwa huu kuwa kubwa”, akaongeza.
Mmoja wa wakazi
waliojitokeza kupima virusi vya ukimwi yeye na mtoto wake, Zainabu Hamza na
mwanaye, Amina Adamu alisema anafuraha sana baada ya kujitambua afya yake kwani
hiyo ilikuwa mara yake ya tatu hivyo hiyo itamsaidia kuweza kuishi akichukuja
tahadhari zote ili asipate maambukizi.
- MWISHO -
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)