Mtoto wa kijiji cha Mndindi Ludewa akitoka shamba
Ludewa bado madaraja ni ya mbao pamoja kama inavyoonekana pichani
Ludewa bado madaraja ni ya mbao pamoja kama inavyoonekana pichani
UBOVU wa miundo mbinu ni chazo
cha umaskini kwa wakazi wa kata ya Mavanga ,Mundindi na Ibumi
ambazo ni miongoni mwa kata za pembezoni mwa wilaya ya Ludewa mkoani Iringa na Tanzania ambayo pia zinaongoza kwa uzalishaji wa mazao ya chakula.
Tanzania
ipo mbioni kusherehekea miaka 50 ya uhuru wake Desemba 9mwaka huu
huku wananchi walio wengi ambao wanashi pembezoni mwa miji wakiwa bado
mateka wa umasikini wa kipato na kujikuta wakisubiri maisha bora
pasipo matumaini .
Umasikini
unaoendelea kuwakumba wakazi wa pembezoni mwa miji hasa katika
wilayani Ludewa unatoa picha halisi ya wilaya nyingine za Tanzania
ambazo pia zitaungana na watanzania wa vijijini kuadhimisha miaka 0 ya
uhuru kwa kilio cha umasikini wa kipato umasikini ambao umechangia kwa
kiasi wanawake na walemavu kuendelea kunyanyasika zaidi katika
familia zao
Pamoja
na kuwa Tanzania ipo katika harakati za kuadhimsha miaka 50 ya Uhuru
wake ila bado maisha ya wananchi wa kata hizi mbili bado ni ya
kubahatisha na kujikuta wakiwa katika harakati za kujikomboa kutoka
katika dimbwi la umasikini.
Kata
ya Mundishi ni kati ya kata 25 zilizopo Wilayani Ludewa na . Kata hii
kijiografia inapakana na kata ya Mavanga na Mkoa wa Ruvuma upande wa
mashariki, kata ya Madili, Lugarawa na Ludende upande wa magharibi
Wilaya ya Njombe upande wa kaskazini na kata ya Ibumi upande wa kusini
.na ni kata inayoundwa na vijiji vitatu Muhindi, Amani na Njelela. Kata
yenye jumla ya wakazi 8412 ikiwa ni wanawake 4460 na wanaume 3952.
Wakati
kata ya Kata ya Ibumi inapakana na kata ya Ludewa na Mundindi upande wa
kaskazini, inapakana na kata na makao makuu ya Wilaya ya Ludewa upande
wa maghalibi, inapakana na na Luilo na Nkoma ng’ombe upande wa kusini
na mashariki inapakana na Mkoa wa Ruvuma Wilaya ya Mfinga na mto Ruvuma
ndio unaotenganisha maeneo hayo kata yenye vijiji 2 vitongoji 7 na
inajumla ya wakazi 1643.
Pamoja
na kuwa kata hizo zina jumla ya watu zaidi ya 10055 ila bado maisha
ya wakazi wake bado ni kuunganisha kutokana na vikwazo mbali mbali
wanazozipata katika kujinasua kwenye dimbwi la umasikini.
Katika
uchunguzi uliofanywa na timu ya waandishi wa habari wa mtandao wa
jinsia Tanzania (TNGP) katika vijiji hivyo umebaini kwepo kwa safari
ndefu kwa serikali kuwakomboa wananchi hao kutoka katika adui
umaskini.
Wakazi
wa kata ya Ibumi na Mndindi Eleteli Mlelwa na Aletelius Mkolongo
wanasema kuwa kutokana na wilaya hiyo ya Ludewa kuwa na utajiri mkubwa
wa mchuchuma na liganga hawakutegemea kama serikali ingeendelea
kuchelewa kuwafanya wakazi wa kata hizo kuwa na maisha bora .
Anasema
Mlelwa kuwa wanashangazwa kuona maisha yanaendelea kuwa magumu
katika vijiji vyao huku baadhi ya watoto wa kike na alemavu katika
kata yao ya Mndindi wanaendelea kukosa elimu kutokana na umaskini wa
familia zao .
“Hivi
sasa katika kata yetu wananchi wamekuwa wakifanya jitihada mbali
mbali za kujinasua katika dimbwi la umasikini ikiwa ni pamoja na
kuongea kasi zaidi ya kilimo lakini bado miundo mbinu mibovu na
imekuwa ni chanzo cha wao kuendelea kuwa duni na kuwa na maisha ya
kifukara “
Hata
hivyo anasema kuwa sehemu kubwa wanaoathirika zaidi na umaskini
huo ni wanawake ,watoto na walemavu ambao katika maeneo hayo
wamekuwa na kawaida ya kutelekeza familia zao na kukimbilia mijini
kwenda kufanya matumizi mabaya ya fedha kidogo wanazozipata katika
kilimo.
Mlelwa
anasema kuwa ni jambo wa kushangaza kuona watanzania tunaadhimisha
miaka 50 ya uhuru huku wananchi wa vijijini wakiendelea kushuhudia
maisha bora kupitia runinga huku katika maeneo yao bado wananchi
wakiwa katika gereza la umasikini .
Anasema
kuwa bado ni ndoto kwa walemavu na wanawake wa pembezoni mwa
Tanzania kuendelea kunufaika na matunda kiasi ya Taifa hili iwapo
serikali haitaweka mikakati ya wazi ya kuwakomboa wananchi hao wa
vijijini ikiwa ni pamoja na kusogeza masoko ya mazao ,kujenga miundo
mbinu bora ya afya ,elimu na usafiri.
Pia anasema kuwa kata yao inakabiliwa na matatizo mbalimbali ikiwa ni pamoja na :
barabara
kutopitika karibu wakati wote wa masika na barabara ya mkoa bado ni ya
changarawe,ukosefu wa soko la uhakika la mazao ingawa nia mazao ya
chakula na ndio kipato cha wananchi wengi vijijini.
Aidha
anasema kuwa kata hiyo ya Mndindi inaupungufu mkubwa wa watumishi
kwa Idara zote hasa Elimu ya Sekondari hali ni mbaya,Sekondari yetu
inapungukiwa majengo muhimu kama maabara hakuna kabisa, ukumbi wa
mikutano na mitihani hamna, madarasa hayatoshi nyumba za walimu
hazitoshi na mabweni hasa watoto wa kike.
Kuhusu majengo yaliyopo hayana samani kama vitanda, viti meza pia
hakuna umeme ingawa ni tatizo la kitaifa, lakini ndani ya Wilaya yetu
inarasilimali nyingi mfano mito mikubwa na madini ya mkaa, vinawezesha
wananchi wa Ludewa kupata umeme wa kutosha na Inchi nzima,Shule yetu
maalumu inamatatizo mengi hasa majengo hayatoshi kulingana na idadi ya
watoto waliopo na walimu waliopo hawatoshi.Shule haina muhudumu
aliyeajiliwa na ukizingatia na hali ya watoto wanaosoma pale.
Huku afisa mtendaji wa kata ya Ibumi Felix Vichale akidai kuwa huduma za jamii zilizopo ni pamoja na shule za msingi shule Elimu maalumu na Sekondari iliyofikia kidato cha nne mwaka 2010 wakati upande wa afya
afya ni zahanati tatu kila kijiji ipo moja.upande wa mawasiliano kata
ina barabara za Wilaya za vumbi zinazounganisha kila upande wa kata
zinazozunguka kata hii na Barabara ya Mkoa inayoelekea Songea (RUVUMA)
“Wananchi
wa kata hii sehemu ni wakulima na wanafanya biashara kiasi, shughuli
zao ni kilimo cha mazao ya chakula kama mahindi, maharage, njegele,
viazi vitamu, kalanga nk. Na mazao ya biashara ni kahawa, pia wanafuga
ngo’ombe wa kienyeji na kisasa kiasi, mbuzi, kondoo, nguruwe, kuku, na
wanyama wadogo wadogo tuna rasilimali ambazo ni pamoja na ardhi ya kilimo na madini, kata imezungukwa na madini ya chuma, dhahabu na mengine mengi.”
Anasema
kuwa wananchi wa kata ya ibumu kwa kujadiliana na wananchi wa kata ya
Ludewa, mnamo mwaka 20001 walikubaliana kuanzisha kuchimba barabara kila
watu kutoka kwenye kata yao hadi mpakani ambako ni kwenye mto, kata
yako kazi hii ilianza mwaka 2002 kwa mkono na serikali Halmashauri ya
wilaya pamoja na wafadhili na iliendelea hadi ilipoisha mnamo mwaka 2005.
Barabara yenye urefu wa zaidi ya kilometa 50 ilichimbwa kwa ushirikiano wa wananchi Serikali na wafadhili .
Alitaja wafadhili hao kuwa ni kampuni ya MRMO E.GRANITO ya Mbeya,
TASAF na MIMI STEER. Shughuli zilizofanyika ni uchinabji wa barabara
hiyo, ujenzi wa makarvati na ujenzi wa madaraja jumla ya gharama katika
mradi huu ni karibu TSH milioni 700
Wakati kijiji cha Mavanga kata ya Mavanga kutokana na umasikini wa wananchi wa eneo hilo
ambalo linaongoza kwa kilimo cha mahindi ,wameonyesha kushindwa
kumalizia majengo ya shule ya msingi Mbugani na kupelekea moja kati ya
jingo jipya katika shule hiyo kubomoka kabla ya kuanza kutumika .
Shule
hiyo ya Mbugani iliyojengwa kwa nguvu za wananchi kwa zaidi ya
shilingi milioni 5 imebomoka baada ya wananchi kukosa fedha za kununua
bati na saruji na serikali kushindwa kuunga mkono jitihada hizo
Uongozi
wa shule hiyo umesema kuwa kuanguka kwa kuta zote za shule hiyo
kumetokana na serikali ya Halmashauri ya wilaya Ludewa kuchelewa
kuunga mkono jitihada za wananchi wa kijiji cha Mavanga ambao
walilazimika kujitolea kujenga shule hiyo ili kuepusha msongamano
wa wanafunzi katika shule moja iliyopo kijijini hapo.
Kaimu
mkuu wa shule hiyo Alemaatema Ngalalikwa anasema kuwa shule
hiyo imeshindwa kuanza kutokana na jingo moja lenye vyumba viwili
vya madarasa kubomoka kwa kukosa bati na saruji na kupelekea shule
hiyo kuendelea kusimama bila kupokea wanafunzi.
Hata
hivyo alisema kuwa wazo la kujenga mkondo huo mpya wa shule ya
Mbugani kulitokana na kikao kilichoketi mwaka 2008 kutathimini
tatizo la utoro wa wanafunzi na msongamano wa wanafunzi hao
madarasani na kuazimia kujenga majengo hayo.
Alisema
kuwa ujenzi huo ulianza toka mwaka 2009 baada ya wananchi
kujitolea kufyatua tofali na kusongeza mawe na kuwa mwaka huo huo
ujenzi ulikamilika na jumla ya shilingi zaidi ya milioni 5 ndizo
zilitumika kujenga majengo hayo ambayo baadhi tayari yamebomoka .
Mbali ya kubomoka kwa majengo hayo pia alisema hata vyumba viwili vya madarasa vilivyosalia katika eneo hilo
vipo hatarini kubomoka kutokana na kutosakafiwa kwa saruji na kuwa
iwapo serikali itachelewa kusaidia kutoa fedha za kukamilisha
ujenzi huo upo uwezekano wa nguvu za wananchi na fedha hizo zaidi ya
milioni 5 zilizotumika katika ujenzi huo kupotea.
Pia
alisema tatizo la madawati ni kubwa katika shule hiyo mpya ambayo
ilitarajiwa kuombewa kibali kwa ajili ya kupunguza wanafunzi kutoka
mkondo mama na kuanzishwa kwa shule hiyo na kuwa hadi sasa hakuna
dawati hata moja katika vyumba hivyo vya madarasa.
Maria
Ngatunga ni afisa mtendaji kata ya Mavanga ambaye alithibitisha
kuwepo kwa tatizo la kubomoka kwa madarasa hayo kutokana nna kukosa
mchango wa serikali katika kukamilisha ujenzi huo na kuwa kwa sasa
tayari Halmashauri iimeazimia kuchangia fedha za kukamilisha ujenzi
huo baada ya kutokea kwa maafa hayo ya majengo kubomoka.
Kwa upande wake mbunge wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe
mbali ya kuwapongeza kwa ujenzi wa shule hiyo mpya ambayo kwa
sasa majengo yake yameanza kubomoka bado aliahidi kujitolea kuchangia
bati 104 ili kuenzeka majengo hayo mara yatakapojengwa upya pamoja na
kjmwomba ofisa elimu kuchangia saruji.
Mbunge
Filikunjombe anasema kuwa njia pekee ya wananchi hao kukikwamua
kiuchumi ni pamoja na kutunza ardhi yao na kuepuka kuuza ardhi kwa
wageni ambao wamekuwa wakifika katika maeneo hayo na kutaka ardhi ili
kugeuza wilaya hiyo ni sehemu ya kuchuma na kuondoka.
Filikunjombe
ambaye kitaalum ni mwanahabari na makamu mwenyekiti wa kamati ya
bunge hesabu za mashirika ya umma (POAC) anasema kuwa vipaumbele vyake
katika wilaya hiyo ni pamoja na kuona ujenzi wa barabara ya lami
unaanza katika wilaya ya Ludewa ambayo kwa sasa haina hata robo
kilometa ya lami na kipaumbele cha pili ni uchimbaji wa makaa Liganga na
mchuchuma.
Anasema
kuwa tatizo la umasikini wa wananchi katika wilaya ya Ludewa ni pamoja
na rasilimali za wilaya hiyo kushindwa kutumika vema na kuwa iwapo
rasilimali hizo zitatumika vema milango ya umasikini kwa wananchi wa
vijiji vya wilaya hiyo itafungwa na kufunguliwa ile ya uchumi.
Imeandaliwa
na Francis Godwin mwenyekiti wa waandishi wa habari wa mtandao wa
jinsia Tanzania (TGNP) mikoa ya kusini mwa Tanzania na mmiliki wa
mtandao Wa Francis Godwin Blogu na mwandishi wa gazeti la Tanzania Daima mkoa wa Iringa.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)