Ofisa
Uhusiano wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Dorris Malulu (wa pili
kulia), na Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Iringa, Pindi Chana (CCM),
wakimtwisha ndoo ya maji Mama Mkazi wa Kijiji cha Lugarawa, Mary Luoga
wakati wa uzinduzi wa tenki la maji lenye ujazo wa lita 50,000
lililojengwa kwa msaada wa Sh. milioni 15 za TBL katika kijiji hicho
kilichopo wilayani Ludewa, Iringa.Makabidhiano ya tenki hilo
yalifanyika hivi karibuni katika kijijini hapo.
Mwenyekiti
wa Bodi ya Shule ya Sekondari Lugarawa, Mathias Kihaule (kushoto),
akiipongeza Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia kwa Ofisa Uhusiano wa
kampuni hiyo, Dorris Malulu baada ya kukabidhiwa mradi wa Tenki la
maji lenye ujazo wa lita za maji 50,000 lililojengwa kwa msaada wa sh.
milioni 15 za TBL katika Kijiji cha Lugarawa, wilayani Ludewa, Iringa.
Anayeshuhudia makabidhiano hayo yaliyofanyika hivi karibuni katika
Kijiji hicho, ni Mbunge wa Viti Maalum, Pindi Chana (CCM).
Mbunge
wa Viti Maalum Mkoa wa Iringa, Pindi Chana (CCM),wa pili kushoto,
Ofisa Uhusiano wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Dorris Malulu (wa tatu
kushoto), Ofisa Tawala wa wa Wilaya ya Ludewa,Charles Keiya na
Mwenyekiti wa Bodi ya Shule ya Sekondari ya Lugarawa, Mathias Kihaule
(kushoto) wakifurahia wakati TBL ilipokabidhi tenki la maji lenye ujazo
wa lita 50,000 za maji katika Kijiji cha Lugarawa, wilayani Ludewa
hivi karibuni.Ujenzi wa tenki hilo umegharimu sh.milioni 15
zilizotolewa na TBL.
Doris Malulu wa TBL, akihutubutubia katika makabadhiano hayo.
Kwaya ya Umoja wa Wanawake wa CCM, wa Kata ya Lugarawa wakitumbuiza katika hafla hyo
Wakazi wa Kata ya Lugarawa wakitumbuiza kwa ngoma wakati wa makabidhiano hayo.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)