MDAU WA MUZIKI WA DANSI NCHINI ISIHAKA KIBENE AFARIKI DUNIA - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

MDAU WA MUZIKI WA DANSI NCHINI ISIHAKA KIBENE AFARIKI DUNIA

Marehemu Isihaka Kibene wa pili kutoka kushoto amefariki dunia leo Jijini Dar es Salaam mara baada ya kuugua kwa muda mrefu.Habari hizo zimetolewa na Ofisa Habari Tawi la Simba Shibam Magomeni Mao Lofombo.Katika enzi za uhai wake Kibene alikuwa ni Mkurugenzi wa bendi inayoundwa na walemavu wa viungo iliyokwenda kwa jina la TUNAWEZA BAND, pia marehemu Kibene alikuwa na mchango mkubwa kwa wanamuziki wa muziki wa dansi wengi wa hapa Tanzania ikiwa ni pamoja na bendi kama Twanga, Mchinga Sound, Extra Bongo, Msondo , Sikinde.
Pia atakumbukwa kwa mengi mazuri.Msiba uko nyumbani kwa Marehemu maeneo ya Ujiji Mwananya Dar es Salaam ambako mipango ya mazishi inafanyika.
Bongoweekend inawapa pole wadau wote wa muziki pamoja na familia ya marehemu.Inna Lillah Wainna Ilaih Rajiun.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages