KANSELA ANGELA MERKEL ATANGAZA KUSAIDIA KUKABILIANA NA UKAME AFRIKA MASHARIKI! - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

KANSELA ANGELA MERKEL ATANGAZA KUSAIDIA KUKABILIANA NA UKAME AFRIKA MASHARIKI!

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel ametangaza kuwa serikali yake itachangia pesa kusaidia juhudi za kukabiliana na ukame Afrika Mashariki.
Bi Merkel amesema Ujerumani itatoa Euro 1 million katika mfuko wa kusaidia walioathirika na njaa katika ukanda wa Afrika Mashariki.

Kulingana na Umoja wa Mataifa zaidi ya watu milioni 10 wanakabiliwa na njaa kufuatia kipindi kirefu cha ukame na wanahitaji misaada ya dharura.Walioathrika zaidi ni raia wa Somalia, nchi ambayo imekumbwa na vita kwa zaidi ya miaka 20.

Kansela wa Ujerumani ametangaza mchango huo katika mkutano kati yake na Rais Mwai Kibaki mjini Nairobi ambapo ameanza ziara rasmi ya nchi tatu barani Afrika.Picha Na East Africa Blogu

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages