Mke
wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda akihutubia baada ya kuzindua meli ya
Ocean Rig Poseidon kwenye bandari ya Geoje nchini Korea ya Kusini Julai
8, 2011.
Mke
wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda akizindua meli ya Ocean Rig Poseidon
kwenye bandari ya Geoje nchini Korea ya Kusini Julai 8, 2011.
Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda na mkewe Tunu wakiwa katika mzungumzo na viongozi
waandamizi walioshiriki katika uzinduzi wa meli ya kukufanyia utafiti
wa mafuta na gesi katika pwani ya Mtwara na Mafia kabla ya uzinduzi
uliofanywa na Mama Tunu Pinda katika mji maarufu wa uundaji meli wa
Geoje nchini Korea Kusini Julai 8,2011
Mke
wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda akiongozwa kukagua meli ya Ocean Rig
Poseidon baada ya kuizindua kwenye bandari ya Mji maarufu kwa ujenzi wa
Meli kubwa wa Geoje nchini Korea ya Kusini Julai 8, 2011. Meli hiyo
inayomilikiwa na kampuni ya Petrobas ya Brazil inatarajiwa kufanya
utafiti wa mafuta na gesi kwenye pwani ya mtwara na Mafia miezi michache
ijayo.
Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda akikagua meli ya Ocean Rig Poseidon baada ya meli
hiyo kuzinduliwa na Mama Tunu Pinda kwenye Bandari maarufu kwa ujenzi
wa meli kubwa ya Mji wa Geoje nchini Korea Kusini Julai 8, 2011.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)