Aliyekua Mbunge wa Igunga-CCM Rostam Aziz
--
HOTUBA YA MHE.ROSTAM AZIZ KWA WAZEE WA IGUNGA TABORA LEO

UTANGULIZI
WAZEE wangu, kwanza kabisa kabla ya kueleza kile ambacho kimenisukuma kuzungumza nanyi leo,napenda kuanza kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu,mwingi wa rehema kwa kutuwezesha kufikia siku hii ambayo inatukutanisha waja wake.
Wazee wangu wa Igunga,baada ya kufanya hivyo napenda pia kutumia fursa hii kuwashukuru ninyi nyote mmoja mmoja na katika umoja wenu kwa kuitikia wito wangu,kijana wenu, niliyewaomba nije nizungumze nanyi siku hii ya leo.
Nafanya hivyo nikitambua vyema kwamba,kama si nyinyi wazee wangu na wengine wengi ambao hatuko nao hapa leo kwa sababu mbalimbali, ambao mmekuwa na imani kubwa nami nisingeweza kufikia hapa nilipofika sasa.
Wazee wangu, waasisi wa taifa letu walitufundisha kutambua na kuheshimu ukweli kwamba; ‘Uongozi ni Dhamana’dhana ambayo kila ninapokaa na kutafakari huwa inanirejesha nyuma na kukumbuka jinsi nyinyi mlivyokaa katika umoja wenu na kuniteua mimi, miongoni mwa vijana wenu wengi, kuwa mwakilishi wa Jimbo la Igunga tangu mwaka 1994.
Katika kipindi hicho chote cha utumishi wangu,nyinyi wazee wangu mmekuwa mhimili muhimu ambao umeniwezesha kutimiza wajibu wangu kwa bidii kubwa, maarifa na nidhamu ya hali ya juu nikitambua namna ambavyo mmekuwa na imani kubwa juu yangu.

Kwa Story Zaidi <<< BOFYA HAPA >>>
damn it!!wengine wafuate nyayo haraka.we are tired of them MAFISADI WAKUBWA.
ReplyDeleteRAY MAUKI wa MWENGE DAR ES SALAaM