Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akisoma hotuba ya ufunguzi wa Mkutano wa mkuu wa tatu wa Baraza la
Wakuu wa Vyuo Vikuu huria Afrika wa siku tatu kuhusu Elimu ya mafunzo ya
Masafa uliofunguliwa lei Julai 13 kwenye Ukumbi wa Mlimani City Dar es
Salaam na kuhudhuriwa na washiriki kutoka nchi mbalimbali za Afrika.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Balozi wa Zambia nchini, Mavis Lengalenga, baada ya kuzindua rasmi mkutano mkuu
wa 3 wa Baraza la Wakuu wa vyuo Vikuu huria Afrika wa siku tatu,
uliofunguliwa leo Julai 13 kwenye Ukumbi wa Mlimani City Dar es Salaam.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt.Mohammed Gharib Bilal,
akisalimiana na baadhi ya washiriki wa mkutano mkuu wa 3 wa Baraza la
Wakuu wa Vyuo Vikuu huria kutoka Afrika baada ya kuzindua mkutano huo
kuhusu mafunzo ya Elimu ya Masafa, leo Julai 13 jijini Dar es Salaam.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akisalimiana na Mhadhiri Chuo Kikuu Huria cha Zanzibar Tanzania, Grace
Kissassi, wakati alipokutana naye baada ya kufungua rasmi mkutano mkuu
wa 3 wa Baraza la wakuu wa Vyuo Vikuu huria kutoka Afrika, kuhusu elimu
ya mafunzo ya masafa uliofunguliwa rasmi leo Julai 13,
2011 kwenye Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam. Kushoto ni
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dkt. Shukuru Kawambwa.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa mkutano huo wa
siku 3, kuhusu mafunzo ya Elimu ya Masafa unaowashirikisha wakuu wa Vyuo
Vikuu Huria kutoka nchi za Afrika, uliofunguliwa leo kwenye Ukumbi wa
Mlimani City Dar es Salaam.
Picha na Muhidin Sufiani-Ofisi Ya Makamu wa
Rais
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)