Kigoda
cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, kilichozinduliwa leo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akisoma hotuba wakati wa hafla ya uzinduzi wa Kumbukumbu ya Kigoda cha Mwalimu
Nyerere kinachohusika na masuala ya Mazingira na mabadiliko ya Tabianchi,
kilichozinduliwa leo Julai 11, 2011 Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na kutangazwa kwa
Mwenyekiti wa kwanza wa Kigoda hicho, Prof.
Pius Yanda
Makamu
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Rwekaza Mukanda (kulia) akimvisha kofia
na Joho, Prof. Pius Yanda, baada ya kutangazwa kuwa Mwenyekiti wa kwanza wa
Kigoda cha Kumbukumbu ya Mwalimu yerere, wakati wa hafla ya uzinduzi wa kigoda
hicho kilichozinduliwa kwenye Ukumbi wa Nkurumah Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
leo Julai 11, 2011. Kushoto ni Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Taalum, Prof. Makenya
Maboko.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akimpongeza Prof. Pius Yanda, baada ya kutangazwa na kuvishwa Joho la kuwa
Mwenyekiti wa kwanza wa Kigoda cha kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, Mazingira na
Mabadiliko ya Tabianchi, wakati wa hafla ya uzinduzi wa Kigoda hicho uliofanyika
leo Julai 11, 2011 katika ukumbi wa Nkurumah Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
Mwenyekiti wa kwanza wa Kigoda cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, Prof. Pius
Yanda, akiwa ameketi kwenye Kigoda hicho baada ya kutangazwa rasmi wakati wa
uzinduzi huo.
Baadhi
ya wageni waalikwa na Mabalozi waliohudhuria hafla hiyo ya uzinduzi.
Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akikagua
maonyesho ya vitabu vya kumbukumbu nje ya ukumbi wa Nkurumah Chuo Kikuu
cha Dar es Salaam baada ya kuzinduz Kigoda cha Kumbukumbu ya Mwalimu
Nyerere leo mchana.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akiagana na baadhi ya Maprofesa wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, baada ya
uzinduzi wa Kigoda cha Mwalimu Nyerere, kilichozinduliwa leo Julai 11, 2011,
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Picha na Muhidin Sufiani-OMR
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)