Mwanamuziki
mahiri wa miondoko ya Hip hop ambaye pia ni muigizaji wa Filamu kutoka
nchini Marekani ajulikanae kwa jina la Christopher Brian Bridges
aliyezaliwa mnamo Septemba 11, 1977,ambaye pia anajulikana zaidi kwa
jina la kisanii kama Ludacris, anatarajiwa kushuka nchini Tanzania na
kuangusha bonge la shoo kwenye tamasha la miaka kumi ya msimu wa dhahabu
unaoendelea na serengeti Fiesta 2011.
Akizungumza na kuthibitisha ujio wa Mwanamuziki huyo mapema leo asubuhi jijini Dar,Mkurugenzi wa Maendeleo na Utafiti wa Clouds Media Group,Ruge Mutahaba amesema kuwa,Mwanamuziki Ludacriss na mwanamuziki mwingine wa kimataifa kutoka nje (atatajwa hapo baadaye),wanatarajiwa kutumbuiza kwenye tamasha la miaka kumi ya msimu wa dhahabu unaoendelea na serengeti Fiesta 2011 kwenye viwanja vya Lidaz Club,Kinondoni jijini Dar Es Salaam mnamo Julai 30.
Mutahaba amesema kuwa mpaka sasa mambo yanakwenda sawa bin sawia,na kwamba shamra shamra za kufikia kilele cha miaka 10 ya Serengeti Fiesta 2011 itakuwa tofauti na wenye msisimko mkubwa ikilinganishwa na miaka mingine yote iliyowahi kufanyika tamasha hilo, ambalo ni kubwa katika anga ya burudani ndani na nje ya Tanzania ikiwemo Afrika Mashariki kwa ujumla.

Aidha Mutahaba amebainisha pia kwa kutoa shukurani za dhati kwa mikoa
ambayo tayari tamasha hilo limekwishafanyika,amewashukuru kwa
kujitokeza kwao kwa wingi na kuonyesha ni namna gani tamasha hilo
linalowakutanisha watu wa aina mbalimbali na linavyowajengea upendo wa
umoja na mambo mengine mbalimbali ikiwemo na kufahamiana.
Mutahaba ameongeza kwa kutoa shukurani nyingi zaidi kwa wakazi wa
Mkoa wa Iringa na Mbeya kwa namna walivyojitokeza kwa wingi na
kulikubali tamasha hilo ambalo hufanyika mara moja kwa mwaka. “Fiesta ya
mwaka huu tumepata sapoti kubwa kutoka kila kona kwa asilimia
kubwa,tunamshukuru kamanda wa polisi mkoani Mbeya Kamanda Nyombi,Kamanda
wa polisi Mkoani Iringa ikiwemo na halmashauri zote mbili
zilizoshiriki kwa namna moja ama nyingine na kulifanikisha tamasha la
Fiesta 2011 kufanyika katika mikoa hiyo”.Alitanabaisha Mutahaba.
“Nisiache pia kuwashukuru wasaniii wote walioshiriki kwenye Mikoa ya
Mbeya na Iringa,kwa pamoja nadhani tuko pamoja katika kuijenga Fiesta
2011.Kutokana na ujio wa Wasanii wa Kimataifa kwa sasa timu yetu inaanza
kujigawa kwa ajili ya kuweka umakini katika kilele cha tamasha hilo
litakalofanyika Julai ,30 katika viwanja vya Lidaz Club.Katika
shamrashamra hizo za kutimiza miaka 10 ya Serengeti Fiesta 2011
kutakuwepo na mambo mbalimbali yatakayolinogesha tamasha hilo kubwa hapa
Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla”,alisema
Wiki hii tamasha la Serengeti Fiesta 2011 litakuwa ndani ya wakazi wa
mji wa Moshi na Arusha,hivyo wajiandae kujiachia na kupata Majotroozzz
ya uhakika kabisa.
Source: G5 NEWS
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)