IGP
Mwema akijibu maswali mbalimbali wakati wa uzinduzi wa kuanza kuhakiki
silaha nchini, uvaaji helmeti na uhamasishaji jamii kutii sheria bila
kusurutishwa
Kamishna wa Polisi, Clodwin Mtweve akisisitiza jambo katika mkutano huo
Mkuu
wa Oparesheni wa Jeshi la Polisi, Kamishna Paul Chagonja akifafanua
mbamo mbalimbali hasa kuhusu oparesheni iliyotangazwa jana na IGP,
Mwema ya kusalimisha silaha zinazomilikiwa isivyo halali
Mkuu wa kitengo cha Polisi cha Maboresho, Lucas Kusima akielezea kuhusu maboresho mbalimbali yaliyofanywa na jeshi hilo
Mkuu wa kitengo cha upelelezi wa makosa mtandao,Kasala,akielezea jinsi wanavyopambana na uhalifu huo
IGP Mwema akikata utepe kuashiria uzinduzi huo
Mkuu
wa Jeshi la Polisi nchini, IGP, Said Mwema (katikati) akivishwa helmeti
baada ya Taasisi ya Helmet Vaccin Initiative Tanzania, kukabidhi msaada
wa helmeti 500 kwa jeshi hilo, wakati wa hafla ya uzinduzi wa
uhamasishaji jamii kuvaa kofia hizo wakipanda pikipiki, Dar es Salaam
jana katika Makao Makuu ya Jeshi la Polisi.
Mkuu
wa Jeshi la Polisi nchini, IGP, Said Mwema (katikati) akiangalia wakati
Balozi wa Hiari wa Uvaaji wa Kofia nchini, Ritta Poulsen (kulia kwake)
baada ya Taasisi ya Helmet Vaccin Initiative Tanzania, ilipokabidhi
msaada wa helmeti 500 kwa jeshi hilo, wakati wa hafla ya uzinduzi wa
uhamasishaji jamii kuvaa kofia hizo wakipanda pikipiki Dar es Salaam
jana.Picha Zote na Mdau Richard Mwaikenda













No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)