Mwimbaji na mtunzi mkongwe wa nyimbo nchini Marekeni, Chaka Khan (53), yuko nchini Tanzania kwa ajili ya kufanya onesho maalum Jumamosi hii jijini Dar es salaam. Chaka Khan, ambaye ni mwimbaji wa wimbo maarufu wa Ain't Nobody, aliouimba mwaka 1983 na kumpatia sifa hadi leo, ametembelea studio za Clouds Media Group zilizopo Mikocheni mapema leo na kukaribishwa na mkurugenzi wake, Joseph Kusaga. Pichani juu akikaribishwa mjengoni na baadae kupiga picha na Mkurugenzi wa Prime Time Promotions, Juhayna ambaye pia ni mkewe Kusaga, pamoja na binti yao Natalia Kusaga.
Chaka Khan, anapokuwa stejini.
Picha Michuzi Jr na Mtandao.





No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)