26/7/2011SERIKALI
imewataka viongozi wa Mchezo wa Pool table nchini kuwaelekeza
wachezaji wao ili wajue muda muafaka wa kuchezwa kwa mchezo huo jambo
ambalo litawafanya waachane na tabia ya kucheza wakati wa kazi.
Wito
huo umetolewa jana na waziri wa Nishati na Madini William Ngeleja
wakati akikabidhi zawadi kwa wabunge washindi wa mchezo huo zilitotolewa
na Chama Cha Pool Tanzania (TAPA) katika hafla fupi iliyofanyika nje
ya viwanja vya Bunge mjini Dodoma.
Waziri
Ngeleja alisema kuwa hivi sasa mchezo huo umekuwa ukichezwa muda
wowote hasa wakati wa kazi jambo ambalo limewafanya viongozi na baadhi
ya wananchi kuulalamikia kuwa unapoteza nguvu kazi ya taifa.
“Nawaomba
mfikishe ujumbe kwa wachezaji na mashabiki wenu ili wajue muda muafaka
na kupanga ratiba ya kucheza Pool table na si kucheza muda wowote hasa
wakati wa kazi na hivyo kupoteza nguvu kazi ya taifa”, Ngeleja akiwaambia viongozi wa TAPA .
Naye Kapteni wa timu ya
Bunge Idd Azan ambaye ni Mbunge wa Kinondoni aliwapongeza viongozi wa
chama hicho kwa jitihada wanazozifanya za kuutangaza mchezo huo na
kuahidi kuwapa ushirikiano zaidi.
Kwa
upande wake Mwenyekiti wa Chama hicho Isaack Togocho alisema kuwa
anafurahi kuona kuwa wabunge wameupokea kwa moyo mkunjufu mchezo huo na
anaamini kuwa watakuwa mabalozi wao wazuri .
Waliokabidhiwa zawadi ni mshindi wa jumla wa mashindano hayo George Simbachawene ambaye ni Mbunge wa Kibakwe alikabidhiwa zawadi ya ngao na fimbo ya kuchezea POOL na mshindi
wa pili Dkt. Charles Tizeba ambaye ni Mbunge wa Buchosa alipata zawadi
ya fimbo ya kuchezea pia timu ya bunge ilipata zawadi ya ngao kwa
ajili ya kukubali kwao kushiriki mashindano hayo.
Mashindano
hayo yalidhaminiwa na bia ya Safari Lager ilikuwa ni kati ya timu ya
bunge na combine ya TBL na TAPA yalifanyika Jumamosi iliyopita mjini
Dodoma.
Na Anna Nkinda – Maelezo, Dodoma.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)