Naibu waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Aggrey Mwanri akijibu
swali la Mbunge wa Biharamulo Magharibi Dkt. Anthony Mbassa (hayupo
pichani) kuhusu Serikali kugawa maeneo mapya katika wilaya hiyo wakati
wa kipindi cha Maswali na majibu Bungeni leo mjini Dodoma.
Waziri
Mkuu Mizengo Kayanza Pinda kulia akimsikiliza waziri wa Kilimo,
Chakula na Ushirika Prof. Jummanne Maghembe (kushoto) wakati wa kipindi
cha maswali na majibu katika kikao cha Bunge la bajeti kinachoendelea
mjini Dodoma.
Mbunge wa Same Mashariki Anna Kilango Malecela akichangia bajeti ya wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika kuhusu umuhimu wa wakulima kuuza mazao yao nje ya nchi.
Mbunge wa Jimbo la Nyang’hwale (CCM) (kushoto) Hussein Nassoro Amar
akisalimiana na Patrick Grones (kulia) ambaye ni Mwalimu wa Shule ya
Sekondari St. Ignatius Collage ya Mjini London Nchini Uingereza nje ya
viwanja vya Bunge mjini Dodoma. Wanafunzi hao wako nchini kwa ajili ya
kujifunza mambo mbalimbali ambapo leo wamepata fursa ya kutembelea
Bunge.
Mbunge wa Mbeya Mjini (CHADEMA) Joseph Mbilinyi akiuliza swali kuhusu umuhimu
wa Serikali kukichukua Kiwanda cha Zana za Kilimo Mbeya ili kukidhi
malengo ya uanzishwaji wake kwenda sambamba na mkakati wa kilimo kwanza
pamoja na kuongeza ajira kwa wananchi wa mkoa huo.
Waziri
wa Katiba na Sheria Celina Kombani (kulia) na Mbunge wa viti Maalum
(CHADEMA) Suzan Kiwanga (kushoto) wakimsikiliza Mbunge wa Maswa
Magharibi (CHADEMA) John Shibuda nje ya viwanja vya Bunge mjini Dodoma
leo mara baada ya kumalizika kwa kipindi cha maswali na majibu.Picha Na Anna Nkinda - Maelezo
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)