Kocha Wa Arsenal Arsenal Wenger
Msimu wa mwaka 2010/2011 ulimalizika kwa huzuni
mkubwa kwa Arsenal. Hii ni klabu ambayo matarajio na matumaini ya
meneja wake pamoja na wachezaji yalikuwa makubwa na kuyatiririsha kwa
mashabiki kupitia ahadi za mambo mazuri kutarajiwa kutoka kwa kikosi
madhubuti.
Lakini baada ya kukosea bila
kudhania kuwa wangeshindwa na Birminham City kwenye fainali ya Kombe la
Carling, klabu ambayo kabla ya hapo ilikuwa ikibabaisha matokeo katika
Ligi kuu.
Tangu hapo Arsenal haikuwa na
ile mori iliyokuwa nayo hapo kabla ikipoteza mchuano wa kombe la FA
dhidi ya mahasimu wao wakuu Manchester United.
Vivyo
hivyo maradhi yakazidi kuikumba klabu hiyo iliyodhibiti nafasi ya pili
na kuonekana yenye fursa kuipiku Manchester United kabla ya kudorora na
hatimaye kumaliza Ligi katika nafasi ya nne.
Kwa Habari Zaidi <<<< BOFYA HAPA >>>>
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)