WATUMIAJI WA MITANDAO YA MAWASILIANO WAFIKIA ZAIDI YA MILIONI TANO - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

WATUMIAJI WA MITANDAO YA MAWASILIANO WAFIKIA ZAIDI YA MILIONI TANO


Watumiaji wa mitandao ya mawasiliano nchini wameongezeka na kufikia Idadi ya watu millioni 5 licha ya makampuni yanayotoa huduma hizo kukabiliwa na changamoto mbalimbali likiwemo suala la miundo mbinu hapa nchini.

Akifungua mkutano wa wadau wanaojishugulisha na masuala ya mitandao Barani Afrika Jijini DSM Katibu mkuu Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Dakta FLORENCE TURUKA amesema Watanzania bado wanayo fursa ya kujifunza namna kutumia mitandao ya mawasiliano.
Kwa upande wake mkurugenzi mkuu wa Mamlaka ya mawasiliano Profesa JOHN NKOMA amesema pamoja na idadi ya watumiaji wa mitandao kuongezeka kwa kasi lakini bado changamoto za matumizi mabaya ya mitandao hiyo ikiwemo uhalifu.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages