Afisa
Mtendaji Mkuu wa Hospitali ya CCBRT Erwin Telemans kushoto akipokea
kutoka kwa Afisa Mkuu wa Masoko wa Kampuni ya Vodacom Tanzania Mwamvita
Makamba mkataba wa Vodacom kuchangia shilingi milioni arobaini katika
ujenzi wa wodi ya wanawake na watoto kwenye hospitali maalum ya wanawake
ya CCBRT Boabab itakayojengwa jijini Dar es salaam.Kulia ni Meneja
Mahusiano wa CCBRT Kira Thomas .
Afisa
Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa Vodacom Tanzania Mwamvita Makamba
(kulia) Mkuu wa Vodacom Foundation Yessaya Mwakifulefule wakimwangalia
Afisa Mtendaji Mkuu wa Hospitali ya CCBRT Erwin Telemans (kushoto)
akisoma mkataba wa makabadhiano ya shilingi Milioni Arobaini kutoka
Vodacom zitakazotumika katika ujenzi wa jengo la wanawake na watoto
katika Hospitali ya CCBRT Baobab itakayojengwa jijini Dar es Salaam.
--
Kampuni
ya simu za mkononi ya Vodacom,kupitia kitengo chake cha kusaidia jamii
cha Vodacom Foundation imekabadhi shilingi milioni arobaini kwa
taasisi ya CCBRT kuchangia ujenzi wa hospitali ya Baobab ambayo itakuwa
ni maalum kwa huduma za afya za wanawake na watoto.
Mkataba
wa makabidhiano umetiwa saini jijini Dare s salaam kati ya Afisa Mkuu
wa Masoko na Mahusiano wa Vodacom Mwamvita Makamba na Ofisa Mtendaji
Mkuu wa CCBRT Erwin Teleman ambapo wote kwa pamoja wamezungumzia mradi
huo wa ujenzi wa hospitali na matumani ya siku za baadae katika kusaidia
wanawake na watoto.
Akizungumza
katika hafla hiyo Mwamvita amesema suala la Tanzania kuendelea kuwepo
katika orodha ya nchi kumi zinazoongoza kwa vifo vya akina mama
linapaswa kupiganiwa kwa pamoja na wadau wote ili kunusuru maisha ya
wanawake na wataoto.
Amesema
Vodacom ni kampuni inayoguswa na ustawi wa maisha ya watanzania na ni
imani ya kampuni hiyo kwamba ujenzi huo utawagusa wadau wengine na
kuchangia kukamilisha lengo huku akiipongeza CCBRT kwa mchango wake wa
kusaidia upatikanaji rahisi na wa gharama nafuu wa huduma za afya
hususan kwa makundi yenye uhitaji maalum.
“Kwa
kweli inauma sana kuona wanawake wa kitanzania wakipata shida ya
huduma za afya serikali imekuwa ikichukua juhudia mbalimbali
kukabiliana na changamoto hii pamoja na taasisi za afya kama CCBRT zote
hizo hazina budi kuungwa mkono na kuongezewa nguvu ili taifa liweze
kukabiliana kwa ukamilifu na changamoto hiyo”Alisema Mwamvita.
Amesema
Vodacom itaendelea kuisaidia CCBRT katika azma yake ya kutoa huduma
bora na rahisi kwa jamii za watazania katika nyanja ya huduma za afya
huku akitoa wito kwa wadau wengine kujiotokeza na kuchangia mradi huo wa
ujenzi wa hospitali.
“Leo
tunakabidhi shilingi milioni arobaini ambazo ni ahadi tuliyoitoa
kuitikia wito wa Rais Jakaya Kikwete wakati alipoongoza harambee ya
kuchangia fedha za mradi huu wa hospitali ya wanawake na watoto lakini
Vodacom haitoishia hapa tutaendelea kuwa karibu na nyie na kuwahamaisha
pia marafiki zetu nao kuwaunga mkono ili lengo litimie”Aliongeza
Mwamvita.
Mwamvita
amesema afya ni miongoni mwa vipaumbele vya kampuni ya Vodacom katika
kusaidia jamii na ndio maana eneo la afya hutengewa zaidi ya asilimia
arobaini ya bajeti kwa mwaka zinazotumika kujenga wodi na ukarabati wa
miundombinu ya hospitali na vituo vya afya vijijini.
Kwa
upande wake Ofisa Mtendaji Mkuu wa CCBRT Erwin Teleman amesema mradi
huo ni wa ubia kati ya serikali na CCBRT na kwamba unalenga kupunguza
vifo vya akina mama na watoto wachanga wanaozaliwa vinavyosababishwa na
changamoto za afya ya uzazi nchini.
“Haifurahishi
kuona wanwake wakirudishwa vijijini wakiwa kwenye maejeneza kwa sababu
ya huduma za afya hasa za uzazi hili halivumiliki na tunataka kuona
wanawake wakifurahia maisha serikali imetupatia ardhi na kuahidi vifaa
tiba CCBRT inasimamia ujenzi na baadae menejementi ya hospitali pamoja
na utoaji wa huduma.Alisema Teleman
Amesema
ujenzi unatarajiwa kuanza wakati wowote kwa kuwa kazi ya ubinfu na
michoro imeshakamilika huku akisishukuru Vodacom kwa kkuwaunga mkono
katika mradi huo.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)