SIMBA ILIPOBANWA MBAVU NA VITAL O YA BURUNDI - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

SIMBA ILIPOBANWA MBAVU NA VITAL O YA BURUNDI

Haruna Moshi katika mechi ya jana

Na Dina Ismail Blogu 

SIMBA SC, jana ililazimishwa sare ya bila kufungana na Vital’O ya Burundi katika mchezo rasmi wa ufunguzi wa michuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Castle Kagame Cup kwenye Uwanja wa, Taifa, Dar es Salaam.

Hata hivyo, kwa sare hiyo, Simba itabidi wajilaumu wenyewe kutokana na kuipoteza nafasi nyingi za wazi za kupata mabao, ingawa na wapinzani wao pia walipoteza.



OCEAN VIEW VINARA KUNDI A
 
WAWAKILISHI wa Zanzibar katika Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Castle Kagame Cup, Zanzibar Ocean View jana walianza vema michuano hiyo, baada ya kuwanyuka Enticelles ya Rwanda mabao 3-2 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Matokeo hayo, yanaifanya timu hiyo iongoze Kundi A, kutokana na wenyeji Simba jana kulazimishwa sare ya bila kufungana na Vuital’O ya Burundi, hivyo kujiwekea mazingira mazuri ya kuingia Robo Fainali.
 
Mabao ya Ocean View jana yalitiwa kimiani na Sabri Ramadhan ‘China’, aliyefunga mawili katika dakika ya pili na 31, wakati la tatu lilifungwa na Suleiman Ally dakika ya 85.
 
Mabao ya wawakilishi hao wa Rwanda, yalitiwa kimiani na Muhile Claver dakika ya 23Manirakiiza Victorie dakika ya 40.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages