Serikali
inawashauri wananchi wote kujenga tabia ya kuandika wosia wakati wa
uhai wao ili kuepusha usumbufu unaoweza kutokea wakati wa kufuatilia
kesi za mirathi na kusababisha watoto wao kuishi maisha ya taabu na
kuongeza wimbi la watoto waishio katika mazingira magumu.
Akijibu
swali kwa niaba ya waziri wa Katiba na Sheria, Waziri wa Ushirikiano
wa Afrika Mashariki, Samwel Sitta alisema masuala ya mirathi nchini
hutawaliwa na sheria tatu. Alizitaja sheria hizo kuwa ni za
kimila ambazo hutumika ikiwa marehemu aliishi kwa kufuata mila na
desturi za kabila lake, sheria ya kiislamu ambayo hutumika ikiwa
marehemu alikuwa mfuasi wa dini hiyo na sheria ya Urithi ya India ya mwa
1865 iliyopokelewa na mahakama za Tanganyika na ambayo hutumika ikiwa
marehemu hakuwa muumini wa dini ya kiislamu au hakuwa akifuata mila na
desturi za kabila lake.
Kwa Chanzo Changu Na Habari Zaidi <<<< BOFYA HAPA >>>>
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)