Hussein Bashe
-------
Ombi
Langu kwa wabunge wa chama changu, si kila jambo kulipinga swala la
Posho (sitting allowance) hakuna sababu ya kulivalia njuga na
kulazimisha kulipata,wabunge wanapata Mshahara,posho ya kuwa nje ya
kituo ,posho ya ubunge FEDHA HIZI zinawatosha ukiangalia hotuba ya zito
tunasema pato la mtanzania ni 770,000 lakini kuna asilimia 20% ambao
wanashikilia 42% ya pato la taifa (32trillion) kati ya hizo wakati 20%
ya masikini wa chini kabisa wanashikilia only 7% ya pato la Taifa.
Kwa
mtazamo wangu ikiwa sitting allowance ambayo kwa ujumla wake
ikipunguzwa tuta save 900bn fedha hizi zikiamuliwa kupelekwa katika
sekta ya ELIMU kuondoa kero ya waalimu kuishi madarasani kwa kuwajengea
nyumba, kwa majirani,ama kuondoa kero ya Mabweni ktk shule za kata,ama
kuondoa kero ya MAABARA katika shule za kata,ama kupelekwa katika sekta
ya Afya , tutakuwa kama Taifa tutamaliza tatizo kubwa sana
tutaipunguzia serekali na walipa kodi mzigo wa fedha ambazo haziendi
katika shughuli za maendeleo,Niwaombe wasiitazame hoja imetoka kwa nani
wa chama gani waipokee na kuiunga mkono Mtakuwa mmeitendea HAKI nchi
yetu,na watanzania ambao mustakabali wa maisha yao katika miaka mitano
ijayo upo mikononi mwa serekali ya CCM (cham chetu) hata kama kama
mnaipata kwa mujibu wa sheria na kanuni fanyeni cost benefit analysis
kwa kuliangalia taifa na si nyinyi peke yenu.kama taifa tutfaidika
zaidi fedh hizi msipopokea na kuamua kama bunge zipelekwe katika
shughuli za maendeleo.
Wapo
wabunge ambao wana jenga Hoja ya kwamba Posho hizo zinawasaidia ktk
shughuli za Majimbo, inawezekana inaukweli,lakini kama MFUKO WA
MAENDELEO WA JIMBO ,POSHO YA UBUNGE 5M,ALLOWANCE YA KUKAA NJE YA JIMBO
80,000,MSHAHARA 2M vyote hivi vimeshindwa kukusaidia kuhudumia Jimbo
basi hata hiyo Posho haita weza,naamini mnatuongoza tutawaona si
wabinafsi mkiunga mkono hili kwani mnachpata kwa maisha yenu
kinawatosha.
Itendeeni
haki Nchii hii katika kipindi hiki ambachi ambacho maisha yanazidi
kuwa magumu shilingi inashuka, kuna vijana wenzetu million 11
wanahitaji msaada waliopo mashuleni na vyuoni wanahitaji msaada wenu
mtakuwa mmetenda haki sana kwa kusamehe hicho kidogo,nimuombe Mbunge
wangu aunge Mkono kusamehe hiyo Posho 70,000 ni Tofali 350 za kuchoma
kwa bei ya kule kwetu ,mara siku za vikao ,ni fedha nyingi tutapata
mabweni, maabara,ama fedha hiyo utakuwa umesaidia vijana wengi kulipiwa
ada ktk shule za Kata. Kwahiyo ni vizuri likaungwa mkono jambo hili
ili kuisaida Nchi
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)