MATEJA WA GETI LA LODWARE NGORONGORO CRATER - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

MATEJA WA GETI LA LODWARE NGORONGORO CRATER


Eneo ambalo geti la Lodware ni eneo ambalo lina Nyani wengi. Kwa kipindi kirefu Nyani hawa wamejijengea tabia ya kukwapua vitu mbalimbali ambavyo vinaachwa wazi kwenye magari ya wageni au wakati mwingine kuwapora wageni vitu toka mikononi mwao. Kutokana na ka-tabia haka, mimi hupenda kuwaita Nyani hawa Mateja, nikiwafaninisha na jamaa wa mitaa ya huku mijini wanaokwapua simu na vitu vingine kwenye magari.
Mnapolikaribia geti la Lodware kuna tahadhari za msingi kabisa ambazo inabidi mzichukue kwa pamoja ili kuepusha tafrani ya namna yoyote na hawa mateja. Awali ya yote ni kuhakikisha ya kwamba vioo vya magari vinafungwa na pia roof ya gari inafungwa pia. Mateja hawa hutumia sehemu hizi kuingia ndani na kuchukua kile kitavutia kwenye mboni za macho yao.

Baada ya kufika geti ni vyema kuhakikisha kuwa milango ya magari haiachwi wazi kwani hiyo ni moja ya njia zao kuingia ndani. Pia, hakikisha mgeni haubebi kitu chenye muonekano unaofanana na lunch box. Nyani hawa wanajua kuwa wageni hubeba lunch box kwenye magari na lunch box hizi huwa na chakula kinachowafaa. hicho ndio kitu cha kwanza huwa wanaanza kukiandama kwenye magari. Wanapoona mtu (akiwa nje ya gari) kabeba lunch box au kitu kinachofanan na lunch box, basi mateja hawa hawatasita kumuandama. Mbaya zaidi ni pale mlengwa wao anapokuwa ni mdada au binti. Huwa wanawasumbua sana akina dada (bila kujali rangi au utaifa) kama inavyoonekana katika picha ya kwanza. Pembezoni mwa eneo la kuegeshea magari, kuna kichaka ambacho mateja hawa huenda kujichimbia na kufaidi kile wanachokwapua eneo la parking.
 
Kwa Habari Zaidi <<< GUSA HAPA >>>

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages