Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba yake
wakati wa Kilele cha maadhimisho ya Siku ya Kupiga vita Biashara na
Matumizi ya Madawa ya Kulevya, yaliyofanyika kwenye Viwanja vya Mwembe
Yanga, jijini Dar es Salaam leo Juni 26, 2011.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Tatu
Mapando, ambaye ni mmoja kati ya vijana waliotoa ushuhuda mbele ya
Makamu wa Rais kuhusu matumizi ya madawa ya kulevya, baada ya kuacha
kutumia madawa hayo. Tatu aliwahi kuwa mnenguaji wa muziki wa dansi
katika bendi za Fm, Academia, Diamond Sound, Betta Musica na bendi
kadhaa za jijini kabla ya kuanza kutumia madawa.
Muelimisha Rika kutoka Banda
la Tume ya Kuratibu Udhibiti wa Dawa za Kulevya, Catherine Saoke,
akifafanulia jambo wanafunzi wa Shule ya Msingi, Kilimahewa ya Temeke,
Mubaraka Abdallah na Ally Kionda, kuhusu utofauti na madhara kati ya
dawa ya Cocaine na Heroin, wakati wanafunzi hao walipotembelea Banda
hilo kwenye Kilele cha Maadhimisho ya Siku
ya Kupiga vita Biashara na Matumizi ya Madawa ya Kulevya, yaliyofanyika
kwenye Viwanja vya Mwembe Yanga, jijini Dar es Salaam leo Juni 26,
2011.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo
kutoka kwa Mkufunzi Mwelimishaji wa FIT, Kaweresia Kisanga, wakati
alipotembelea na kukagua mabanda katika Viwanja vya Mwembe Yanga jijini
Dar es Salaam leo, Juni 26, 2011, wakati wa Kilele cha Maadhimisho ya
Siku ya Kupiga vita Biashara na Matumizi ya Madawa ya Kulevya,
yaliyofanyika kwenye Viwanja vya Mwembe Yanga, jijini Dar es Salaam leo
Juni 26, 2011.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo
kutoka kwa Kaimu Mkemia Mkuu wa Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Bertha
Mamuya (katikati) wakati alipotembelea na kukagua mabanda katika
Viwanja vya Mwembe Yanga jijini Dar es Salaam leo, Juni 26, 2011, wakati
wa Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Kupiga vita Biashara na Matumizi
ya Madawa ya Kulevya, yaliyofanyika kwenye Viwanja vya Mwembe Yanga,
jijini Dar es Salaam leo Juni 26, 2011.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo
kutoka kwa Mwelimishaji, Januari Ntisi (kushoto kwake) wa Banda la Tume
ya Kuratibu Udhibiti wa Dawa za kulevya, wakati alipotembelea na kukagua
mabanda katika Viwanja vya Mwembe Yanga jijini Dar es Salaam leo, Juni
26, 2011, wakati wa Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Kupiga vita
Biashara na Matumizi ya Madawa ya Kulevya, yaliyofanyika kwenye Viwanja
vya Mwembe Yanga, jijini Dar es Salaam leo Juni 26, 2011.
Wanafunzi kutoka Shule
mbalimbali za jijini Dar es Salaam, wakipita mbele ya jukwaa la mgeni
ramsi, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed
Gharib Bilal, na mabango yenye ujumbe mbalimbali kuhusu suala zima la
kupiga vita matumizi ya madawa ya kulevya, wakati wa Kilele cha
maadhimisho ya Siku ya Kupiga vita Biashara na Matumizi ya Madawa ya
Kulevya, yaliyofanyika kwenye Viwanja vya Mwembe Yanga, jijini Dar es
Salaam leo Juni 26, 2011.
Kikundi cha Sanaa cha Temeke,
kikitoa burudani wakati wa sherehe hizo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitembelea na kukagua mabanda
katika Viwanja vya Mwembe Yanga jijini Dar es Salaam leo, Juni 26, 2011,
wakati wa Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Kupiga vita Biashara na
Matumizi ya Madawa ya Kulevya, yaliyofanyika kwenye Viwanja vya Mwembe
Yanga, jijini Dar es Salaam leo Juni 26, 2011. Picha na Muhidin
Sufiani-Ofisi Ya Makamu Wa Rais
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)