Na Nova Kambota,
Niliwahi kutabiri huko nyuma kuwa siku Lowassa atakapofungua mdomo
wake na kuzungumza basi hali ya kisiasa ya nchi itabadilika ghafla naam!
Lowassa jana sio tu amezungumza bali amezungumzia sehemu sahihi ambayo
ndiyo haswa alipopaswa kuyasema aliyoyasema, nani kasema kuwa kuna
baadhi ya watu hawajavutiwa na hatua hii ya lowassa? bilashaka kitendo
cha lowassa kusimama upande wa wananchi kwa kuponda utendaji mbovu wa
serikali huku akipandikiza moyo wa kujiamini kama taifa kwa mfano
kutumia pesa tulizonazo kutatua matatizo yetu huku akikazia kwaa
kibwagaizo cha ….“tujenge reli ya kati, tupanue bandari Tanga, DSM, pesa tunazo, tumejenga UDOM kwa pesa zetu wenyewe” hali
iliyofanya baadhi ya wabunge kumpigia makofi, hapa kuna siri kubwa
ambayo inaturudisha kwenye swali lisilojibiwa la TATIZO NI LOWASSA AU
URAIS 2015? sasa mimi nasema hivi Kikwete lete utamu sasa mambo yazidi
kunoga! ila hii ni vita na hainaa macho lazima mmoja ashinde na
mawingine ashindwe hivyo mwisho wa yote haya kuna mmoja atajeruhiwa tu
kisiasa lakini ndiyo hivyo tena hakuna jinsi hii ni safari ya kuwaweka
huru wote wawili JK na Lowassa kwani sasa kwa mbali naona wameanza sfari
ndefu ya kuutafuta UKWELI.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)