Spika
wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Anne Makinda akitoa
ufafanuzi kwa wabunge kuhusu shughuli za kikao cha nane cha mkutano wa
nne wa Bunge leo mjini Dodoma ambapo wabunge mbalimbali wamepata fursa
ya kuchangia bajeti ya serikali ya mwaka 2011/2012 iliyowasilishwa hivi
karibuni na Waziri wa Fedha na Uchumi Mustapha Mkulo.
Mbunge
wa Vunjo na Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Hesabu za
Serikali za Mitaa Augustino Mrema akiingia ndani ya ukumbi wa Bunge
kuhudhuria kikao cha nane cha Bunge leo mjini Dodoma.
Mbunge
wa jimbo la Mtera,Livingstone Lusinde akichangia bajeti ya serikali ya
mwaka 2011/2012 iliyowasilishwa hivi karibuni na Waziri wa Fedha na
Uchumi Mustapha Mkulo na kuhoji uchelewaji wa baadhi ya ofisi za
serikali na Viongozi mbalimbali kuhamia mjini Dodoma ambako ndio makao
makuu ya nchi leo mjini Dodoma.
Picha na Aron Msigwa – MAELEZO.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)