Mheshimiwa January Makamba Mbunge wa Bumbuli-CCM na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini
----------
Na Kizitto Noya, Dodoma
MWENYEKITI wa Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini, Januari Makamba, amesema siyo sahihi kumlaumu Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja na Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), kwa tatizo la umeme nchini.
MWENYEKITI wa Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini, Januari Makamba, amesema siyo sahihi kumlaumu Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja na Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), kwa tatizo la umeme nchini.
Akizungumza mjini hapa jana,
Makamba alisema sekta ya umeme nchini imepita vipindi vitatu tofauti;
kabla ya miaka ya 90 na baada kuanzia mwaka 1996 hadi mwaka 2000, hivyo
suala hilo limekuwa na historia.
“Kimsingi
siyo sahihi kumlaumu waziri wala Tanesco yenyewe, matatizo hayo
yalikuwapo na waziri ameyakuta. Cha msingi kama Taifa, tushikamane na
tuone tatizo hilo kama janga na tuungane kupambana nalo,” alisema
Makamba.
Akifafanua historia hiyo,
Makamba alisema uendelezaji umeme nchini kabla ya mwaka 1996, Tanesco
ilikuwa ikijiendesha kwa ufanisi mkubwa ikiwa inamilikiwa na serikali
kwa asilimia zote.
“Kipindi
kilichofuata ni mwaka 1997 hadi 2006, Tanesco iliwekwa katika orodha ya
mashirika yanayotakiwa kubinafsishwa, lakini hakuna hatua iliyochukulia
hadi mwaka 2006 uamuzi huo ulipobatilishwa,” alisema Makamba na
kuongeza:
“Wakati wote huo ikisubiri
kubinafsishwa, hakuna uwekezaji uliofanyika katika shirika hilo wakati
uchumi wa taifa ulikuwa unaendelea kukua kwa kasi kubwa kufikia kiwango
cha asilimia saba na mahitaji ya umeme, yakiongezeka maradufu.”Kwa
Habari zaidi Bofya na Endelea......>>>>>>
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)