Waziri wa ustawi wa jamii
maendeleo ya vijana wanawake na watoto bi Zainab Omar Mohd
Na
Mwandishi Wetu,Zanzibar
Waziri
wa ustawi wa jamii maendeleo ya vijana wanawake na watoto bi Zainab
Omar Mohd amewaasa wazazi kutowanyanyasa watoto na kuwaomba waheshimu
haki zao za msingi ili wawe wanafamilia na viongozi bora wa baadaye.
Waziri
ameyasema hayo leo katika ukumbi wa bwawani mjini Zanzibar alipokuwa
akizungumza katika warsha ya maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika
ambayo kilele chake hufanyika kila Juni 16 duniani kote.
Katika
kuazimisha siku hiyo ujumbe wa mwaka huu umetajwa kuwa ni “kwa pamoja
tuchukue hatua za haraka ili kunusuru watoto wa mitaani” ambao
wanaonekana kushamiri katika jamii ya Zanzibar.
Akielezea
sababu ya ujumbe huo Bi zainab amesema inatokana na kuongezeka kwa
watoto hao mitaani ambao chanzo chake kimetajwa kuwa ni pamoja na
mifarakano ya ndoa katika jamii.
Aidha
Bi Zainab ameipongeza bodi ya watoto hao kwa utendaji kazi wake pamoja
na kuchangia shl. Mill.1 ambazo zitasaidia uendeshaji wa bodi hiyo.
Naye
Kaimu Katibu Mkuu wa wizara hiyo bw. Mshamu Abdallah khamis ameongezea
kuwa watoto wana haki zao za msingi ambazo wanapaswa kupatiwa ili
watakapokuwa wakubwa waweze kuzisimamia haki hizo kwa wengine.
Katika
warsha hiyo ambayo ilihudhuriwa na wawakilishi wa watoto kutoka sehemu
mbali za Zanzibar, watoto hao walipata fursa ya kutoa maoni yao kwa
serikali ikiwa ni pamoja na kuongeza bajeti katika wizara ya ustawi wa
jamii maendeleo ya vijana wanawake na watoto, ambapo wao ni wadau wa
wizara hiyo.
Siku
ya mtoto wa Afrika ambayo huazimishwa kila ifikapo Juni 16 iliasisiwa
kutokana na mauaji ya watoto yaliyofanyika Afika ya kusini katika eneo
la Soweto mwaka 1976 kutokana na kudai haki yao ya elimu.
Habari kwa Hisani ya Michuzi Blog Via Mbeya Yetu
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)