JUST IN:HATIMAYE UNIVERSITY OF DODOMA (UDOM) KESHO KUGOMA MARA BAADA YA KUAMBIWA RASMI KUWA HAKUNA MAFUNZO KWA VITENDO - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

JUST IN:HATIMAYE UNIVERSITY OF DODOMA (UDOM) KESHO KUGOMA MARA BAADA YA KUAMBIWA RASMI KUWA HAKUNA MAFUNZO KWA VITENDO

Wanafunzi wa Kitivo Cha Sayansi ya Jamii, Sanaa na Lugha wakusanyika Mchana huu Kwaajili ya kuamua maswala mazima ya mafunzo kwa vitendo.
Wanafunzi wakisikiliza kwa makini maelezo yaliyokua yakitolewa na Raisi wa Kitivo cha Sayansi ya Jamii Mh Mwakibinga Philipo Juu Ya Mambo yaliyoweza kufanywa na Serikali mpaka mchana.
Wanafunzi Wa Udom Wakiwa wenye shauku ya kutaka kujua uamuzi utakaochukuliwa na uongozi wa wanafunzi mchana huu katika uwanja wa mpira wa kikapu na mbele ya bweni namba tatu

Wanafunzi Wakitawanyika Mara baada ya Raisi wa kitivo kuwapa uwezo wa kuamua mara baada ya mada iliyotakiwa kuamuliwa na bunge kuwaa tata na kurudishwa kwa wanafunzi ili iweze kuamriwa kama katiba ya serikali ya wanafunzi inavyoeleza
Umati wa wanafunzi ukiwa umekusanyika mbele ya bweni namba tatu na kwenye uwanja wa mpira wa kikapu wakisikiliza maelezo kutoka kwa Raisi wa Kitivo cha Sayansi ya Jamii mchana huu
 Wanafunzi wa Kitivo cha Sayansi ya Jamii, Sanaa na Lugha wakiendelea kusikiliza kwa makini uamuzi utakaoamuliwa na wanafunzi wote.
Wanafunzi wakiwa wametawanyika mara baada ya mkutano huo kutawanyika na kufikia maamuzi ya kugoma.

Na Josephat Lukaza - University of Dodoma (UDOM)

Wanafunzi wa chuo kikuu cha dodoma kitivo cha sayansi ya jamii, sanaa na lugha wamekusanyika mchana huu mbele ya bweni namba tatu na kwenye uwanja wa mpira wa kikapu kwaajili ya kumsikiliza raisi wa kitivo cha sayansi ya jamii Mh Mwakibinga Philipo Kwa ajili y kuelez jinsi ya serikali yake ilivyoweza kufanya yote yaliyowezekana kufanywa na serikali yake na kuwapa wanafunzi wenyewe waamue mara baada ya serikali nzima ya wanafunzi kufuatilia swala hili kwa ngazi husika na kuonekana kuwa hakuna uwezekano wa suluhu iliyoweza kupatika.

Raisi wa Kitivo Cha sayansi Ya jamii, sanaa na lugha Ametubia katiba ya serikali ya wanafunzi wa chuo kikuu cha dodoma UDOSO kuwapa mamlaka wanafunzi ya kuamua mara baada ya bunge kushindwa kutoa maamuzi katiba ya UDOSO inasema mada yoyote ile inayoshindikana kupata suluhu ndani ya kikao cha bunge basi maamuzi yataammuliwa na wanafunzi Mamlaka hayo ya katiba yamewapa wanafunzi uwezo wa kuamua pale bunge linaposhindwa kufikia muafaka.

Wanafunzi Wamefikia Muafaka wa Kugoma hapo kesho Kuanzia Saa Kumi Alfajili Kwaajili ya kwenda bungeni kuonana na Waziri Mkuu Mh Mizengo Pinda Kwaajili ya Kuweza kupata uamuzi juu ya maswala mazima kuhusu mafunzo kwa vitendo kitu ambacho kiliahidiwa na Waziri wa Elimu Shukuru Kawambwa na Waziri Wa Mambo ya Ndani Mh Shamsi Vuai Nahodha Kuwaahidi wanafunzi wa kitivo hiki kuwa wataenda kufanya mafunzo kwa vitendo wakati walipofika kusuluhisha mgomo uliotokea tarehe 20 Disemba 2010 

Katika Usuluhishii huo Waziri Kawambwa Na Shamsi Vuai Nahodha Waliweza kuwaagiza uongozi wa chuo na Tume ya vyuo vikuu Tanzania pamoja na Bodi ya mikopo kufanya mchakato wa haraka kuwezesha wanafunzi ambao hawana mafunzo kwa vitendo wanakwend katika likizo ndefu ambayo inatakiwa kuanza mara baada ya wanafunzi kumaliza mitihani yao ya mwisho wa muhula inayomalizika tarehe mosi julai 2011

Mgomo Huu Mkubwa Ambao umeweza kuhusisha  baadhi yavyombo vya serikali umekuja mara baada ya Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania Kutoa Tangazo kuwa hakuna kwenda kufanya mafunzo kwa vitendo kwa kozi ambazo hazina mafunzo kwa vitendo, tangazo hilo limesababisha wanafunzi, uongozi wa chuo kushangaa uamuzi uliofikiwa na Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania Kwa kutoa tangazo hilo wakati walikuaa wameshakubaliana na Waziri Wa Elimu tayari alishatoa maamuzi.

Zoezi zima la Mafunzo kwa Vitendo lilianza vizuri mara baada ya uongozi wa chuo kutumia gharama kubwa kwaajili ya kuwatumawalimu wwake kusafiri kwenda mikoani kwaajili ya kuomba wanafunzi wakubaliwe kufanya mafunzo kwa vitendo lakini zoezi hilo limezimishwa haraka na Tume ya Vyuo Vikuu tanzania kutoa tangazo la kwamba hakuna Mafunzo Kwa Vitendo.

Taarifa zilizofikia Mtandao huu Wa Lukaza Blog  ni Endapo Wanafunzi Wakigoma siku tatu mfululizo Basi chuo kinafungwa na tetesi Zilizopo Ni kwamba chuo kikifungwa kufunguliwa kwake ni mpaka mwongozo wa wanafunzi ambao ni prospectus kuandikwa upya ili kunusuru migogoro mingine inayohusiana na mafunzo kwa vitendo

Wakati huo wenye daladala ambazo zinafaya kazi yake kati ya chuo kikuu cha dodoma na mjini wamezuiliwa kupandisha kwenda chuo huku nao wakieleza kuwa endapo mgomo utatokea na wanafunzi kufukuzwa chuo na kufungwa basi na wao hawatakuja chuo kubeba abiria.

Mgomo wa Kesho wa Wanafunzi  Wa UDOM umeamuliwa na Wanafunzi wote waliohudhuria Mkutano Huo

Saa Kumi Jioni Ya Leo Uongozi Pamoja na Wanafunzi Wa UDOM watafanya mhadhara Wa wazi WakivialikaVyombo Vya Habari kwa ajilli ya Kuwaeleza Watanzania Kwa kile kilichojili Hapa chuo na hali ilivyokua kuanzia mwanzo hadi mwisho 

Endelea Kutembelea Blogu yenu Kwa Matukio Zaidi.

3 comments:

  1. Anonymous11:19 PM

    jamani muwape haki zao umeona wapi wanafunzi wa chuo bila field acheni hizo fanyeni mpango watoto waende field

    ReplyDelete
  2. Anonymous11:23 PM

    jamani eeeeeeeeeeeeeehhh sio fair tcu pamoja na mawaziri kutoaahadi kumbe walikua wanadanganya kwa hili hata wakijivua gamba hakuna kitu ila haki zetu mtupe

    ReplyDelete
  3. Anonymous11:26 PM

    mmmmhhhhh kazi ipo kwa elimu ya bongo haki yako mpaka muandamane?yataisha lini haya

    ReplyDelete

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages