Wanafunzi Wa Udom Kutoka Vitivo Viwili Cha Sayansi Ya Jamii,
Sanaa na Lugha Pamoja Na Kitivo Cha Sayansi Asilia Wakiwa Wamekutana
Katika Viwanja Vya Nyerere Square Baada Ya Kuwazidi Maarifa Polisi
Waliojitahidi Kuwazuia Barabarani Wakati Wanafunzi Walipita Njia Za
Mikato Hadi Kufika Viwanjani hapo
Mwanafunzi Wa UDOM akiwa amebeba Bango ambalo Linasema
"Pinda Adanganya Tena Must Step Down" Mara Baada Ya Kukutana Katika
Viwanja Vya Nyerere Square.
Mwanafunzi Akiwa Amebeba Bango linalosema
"Bila Field (Mafunzo Kwa Vitendo) UDOM ni Shule
ya Sekondari" Wakati wamekusanyika Katika Viwanja Vya Nyerere Square
Asubuhi Hii
Wanafunzi
Wa Vitivo Viwili Kutoka Chuo KIkuu Cha Dodoma Wakiwa Wamekusanyika
Katika Uwanja Wa Nyerere Square Asubuhi ya Leo Mara baada ya kuwazidi
akili polisi ambao walijipanga kuwazuia wanafunzi hao barabaranii wakati
wanafunzi wakatumia njia za mikato na hatimaye kufika viwanjani hapo
Wanafunzi
Wakimsikiliza Raisi Wa Kitivo Cha Sayansi Ya Jamii Mh Mwakinbinga
Wakati Akitoa Maelekezo Jinsi Ya Kuweza kufika Bungeni Kuonana Na Waziri
Mkuu Na Waziri Wa Elimu
Raisi
Wa Kitivo Cha Sayansi Ya Jamii, Sanaa na Lugha Akitoa Maelekezo Juu Ya
Kufika Bungeni KUonana na Waziri Mkuu
Waandishi Wa Habari kutoka Vyombo Mbalimbali Vya Habari
Wakichukua Habari Wakati Raisi Wa Vitivo hivyo Viwili Wakitoa Maelekezo
Muhimu
Wanafunzi
Walipokua Wakiimba Nyimbo za Ukombozi Pamoja Na Wimbo Wa Taifa Na
Tanzania Tanzania
Maraisi
Wa Vitivo Mh Mwakibinga Wa Sayansi Ya Jamii, Sanaa na Lugha( Wa Kulia)
Na Lema Wa Kitivo Cha Sayansi Asilia Wakiteta Jambo Mara baada Ya kutoa
Maelekezo Kwa Wanafunzi Waliokusanyika Viwanjani hapo
Wanafunzi
Wa UDOM wakijiandaa kuelekea Bungeni Wakitokea Viwanja Vya Nyerere
Square Asubuhi hii
Vijana
Wa IGP Mwema Wakiwa Tayari Nje ya Uzio Wa Nyerere Square Kwaajili Ya
Kuwazuia Wanafunzi Wasifike Maeneo Ya Bunge Lakini Bado Waliweza
Kukubali Kushindwa na Kuzidiwa Maarifa Na Wanazuoni Hao Kwa Kuzidiwa
Maarifa na HAtimaye wanafunzi kuweza Kupita na kukaribia maeneo ya bunge
na hapo ndio mabomu yalipoanzaa kusikika
Askari
Polisi Wakiwa Wamejiandaa Kwa ajili Ya kuwazuia Wanafunzi Hao Lakini
Walionyesha kushindwa kete na wanafunzi kukaribia maeneo ya bunge huku
wengi wakiwa wamefika na Hatimaye mabomu kulindima Maeneo ya Bunge
Kaa Tayari kama Wanavyoonekana hapo wakiwa na shauku ya
kupiga
Hatimaye Polisi Wameweza Kukubali kushindwa na
Kuzidiwa Kete wakati wa kuwazuia Wanafunzi Wasiweze kufika Mjini Dodoma
Kwaajili Ya Kuelekea Bungeni Kuonana Na Waziri Mkuu Mh Pinda Kwaajili ya
kutoa Malalamiko yao kuhusu kufutwa Kwa Mafunzo Kwa Vitendo (FIELD)
kama Walivyokubaliana Mwanzo
Hapo Awali wanafunzi Wa Kitivo Cha Sayansi
Asilia Waliweza Kuwahi Kuamka Na kuelekea Mjini Na Kufanikiwa Kufika
Karibu Na Mjini Lakini Polisi Hao Waliweza Kuwazuia Kwa Muda Lakini Bila
Mafanikio Wanafunzi Waliweza Kugawanyika Makundi na Kupita Njia
Tofautitofauti Na Kukutana Katika Viwanja Vya Mwalimu Nyerere Square
kwaajili ya kujipanga upya
Polisi Kwa Kujua Kuwa Waliowazuia Mwanzo Ndo
Chuo Kizima Na Kusahau Au Bila Kujua Kuwa Kuna Kitivo Kingine Kinakuja
waliweza kuchanganyikiwa ni wapi pa kuwazuia wanafunzi wa kitivo cha
sayansi ya jamii, sanaa na lugha Ambao Walionyesha umahiri wa hali ya
juu wa kuweza kupita njia za mikato hadi kufika mjini pamoja na polisi
wachache kuweza kujua walipopita lakini walishindwa kufika na kupiga
bomu moja la machozi ambalo halikumwasiri mtu yeyote yule
Baada ya
Wanafunzi Hao Wa Vitivo Vyote Viwili Kufanikiwa Kufika Viwanja Vya
Nyerere Square Na Kupanga Mikakati kabambe ya Kuelekea Bungeni Wanafunzi
Hao Walianza Kuondoka Na Kuelekea Bungeni Huku Polisi Wakiwa hawajui
cha kufanya kwa kuzidiwa ujanja HAtiamye polisi Waliweza kuwazuia
Wanafunzi Hao Katika Makutano ya Barabara Ya Standi Kwa Kuwalushia
Mabomu ya Machozi Wakati wanafunzi wanakimbilia sehemu mbalimbali
wanafunzi hao waliweza kukutana tena maeneo ya sokoni ambapo askari
waliweza kuwafuata na kupiga mabomu ya machozi ambayo wanafunzi
walionyesha kuwa walijiandaa na kuanza kunawa kwa maji waliyobeba wakati
wakitoka chuo.
Wakati wanafunzi hao Wakiwa Wametawanyika sehemu
mbalimbali za Mji Wa dodoma Wanafunzi waliweza kuharibu bidhaa za watu
ambao walikua sokini wakati wa kukimbia kwaajili ya kunusuru Maisha yao.
Baada ya Dakika Si Zaidi Ya Kumi na Tano
Wanafunzi Hao waliweza kukutana Tena Viwanja Vya Nyerere Square Na Ndipo
Mkuu Wa Mkoa Dr Msekela Kufika Na Kuwaambia Wanafunzi Kuwa Wasubiri
Waziri Wa Elimu Mh Kawambwa Anakuja Kuongea Na wanafunzi Hao.
Muda
Zaidi Ya Saa Moja Na Nusu Waziri Wa Elimu Hakutokea Na Hatimaye
Wanafunzi Wakaanza Tena Kuimba Nyimbo za Ukombozi Na Hatimaye polisi
Wakafika Tena Viwanjani hapo Na kuwatawanya Wanafunzi hao.
Mpaka Naingia Mitambo Wanafunzi Waliokamatwa
wanafikia 30 huku wengine wakiachiwa na Mpaka Sasa waliopata majeraha
wanakadiriwa kufikia 7 ambapo inasemekana mmoja wa majeraha Hao
Amevunjika Mguu Mara baada ya kupigwa na polisi na Hatimaye kumtelekeza
hapo na ndio wananchi wenye moyo safi kumchukua na Kumpeleka Hospitali
ya Mkoa Wa Dodoma kwaajili ya matibabu
Mpaka Muda huu Inasemekana Waziri Wa Elimu Mh Kawambwa na
Mkuu Wa Mkoa Dr Msekela wamefika Ofisi Za Chuo Kuongea na Viongozi Wa
Juu Wa Chuo.
Lakini Hali inavyoonekana
Hadi muda huu ni kuwa Mgomo Bado unaendelea japokuwa kuna tetesi kuwa
wanafunzi hao wameambiwa warudi chuo kwaajili ya kusubiri Waziri Wa
ELimu Aje kuongea Nao Saa Kumi Lakini Wanafunzi Hao Wanesema Kuwa
Asipokuja na Maelezo ya Kuwa ni Lini Wataenda kufanya mafunzo Kwa
Vitendo na Lini Pesa yao Itaingia kabla ya kufanya Mitihani yao ya
kumaliza Muhula ambayo inaanza tarehe 20 june 2011 Basi Mgomo utaendelea
na ambapo kama wataendelea na mgomo huo hapo kesho watakuwa wamebakiza
siku moja ili chuo kifungwe kutoka na katiba ya TCU na Bunge Kuwa Chuo
Wakigoma Siku Tatu Mfululizo Basi Chuo Kifungwe.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)