JUST IN: SIMBA YAILALUA MOTEMA PEMBE GOLI 1 - 0 UWANJA WA TAIFA - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

JUST IN: SIMBA YAILALUA MOTEMA PEMBE GOLI 1 - 0 UWANJA WA TAIFA

Mchezaji wa timu ya Simba Mussa Hassan Mgosi akiwa amembeba mchezaji mwenzake Amri Kiemba mara baada ya kupachika goli la kwanza na la ushindi, katika goli la timu ya Motema Pembe kutoka DRC kwenye mchezo wa michuano ya Kombe la Shirikisho la CAF, uliochezwa katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam jioni hii, goli hilo limefungwa kipindi cha kwanza dakika ya 20 ya mchezo huo mshabuliaji Mgosi aliipokea pasi nzuri kutoka kwa kiungo Mohamed Banka kufunga goli hilo pekee, hivyo Simba imefanikiwa kuwatoa "ulimi nje" wapinzani wao Motema Pembe ya DRC.
Mchezaji Emmanuel Okwi akimtoka beki wa timu ya Motema Pembe katika mchezo wa Kombe la Shirikisho la CAF katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Mshika kibendera akiangalia wakati wachezaji wa timu ya Simba na Motema Pembe wakichuana katika mchezo wao unaofanyika sasa kwenye uwanja wa Taifa
Mashabiki wa timu ya Simba wakiangalia mchezo huo kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Credits: Full Shangwe Blogu 

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages