BREAKING NEWS: MAKAMU WA MKUU WA CHUO PROF IDRISA KIKULA ATETA NA WANAFUNZI WA UDOM USIKU HUU - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

BREAKING NEWS: MAKAMU WA MKUU WA CHUO PROF IDRISA KIKULA ATETA NA WANAFUNZI WA UDOM USIKU HUU

Makamu Mkuu Wa Chuo Prof Idrisa Kikula Aongea na wanafunzi mbele ya bweni namba tatu kuwaeleza wanafunzi kuhusu ujumbe aliopewa na serikali.
Katika Hali aliyokuwa akielezea Ujumbe aliotumwa Na serikali kuwa serikali imesema kuwa wanafunzi  wataenda kufanya mafunzo kwa vitendo na pesa zitaingia kabla ya kuanza mitihani ya mwisho ambao inatarajiwa kuanzia jumatatu ijayo.

Wanafunzi hao wameonyesha kukataa ujumbe ulioletwa na Makamu Mkuu Wa Chuo Prof Idrisa Kikula na kuendelea kushikilia misimamo yao kuwa kesho mgomo uendelee kwa sababu walishawahi kuahidiwa na Mawaziri Shamsi Vuai Nahodha na Shukuru Kawambwa na Waziri Mkuu Mh Pinda halafu hakuna kitu na kuchukulia hii ni kama siasa na ndio maana wanafunzi wamegoma na wamekataa kukubali ombi lililoletwa na Makamu Mkuu Wa Chuo Prof Idrisa Kikula.

Wakati huo Huo Waziri Mkuu Wa Serikali ya Wanafunzi Amenusurika Kupigwa Kwa kile kinachosemekana amewasaliti Wenzao. Mpaka Muda huu hali si shwari UDOM na Hali bado haijajulikana 
Tuendelee Kuvuta Subira Kujua Kama Kesho Mgomo Hupo Au Haupo.

1 comment:

  1. udom sasa inataka kuweka histori mana hayo mapambano kama kwa gadafi...

    ReplyDelete

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages