JINSI YA KUPIGA KURA KATIKA SHINDANO LA TANZANIA BLOG AWARDS - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

JINSI YA KUPIGA KURA KATIKA SHINDANO LA TANZANIA BLOG AWARDS





Kura zitaanza kupokelewa kwenye blog hii tarehe 25/06/2011 kuanzia saa 12.01AM (saa za Africa ya mashariki)  mpaka tarehe 09/07/2011 saa 11:59PM (tafadhali zingatia muda). Utaweza kupiga kura yako katika kipindi cha wiki mbili.  Tumeamua kuweka muda huo wa wiki mbili ili kuepusha malalamiko ya wale wanaopenda kulalamika tu kwa kila jambo. Tunategemea katika kipindi hicho kila mtu anayetaka kupiga kura ataweza kupiga kura na pia wenye blogs wataweza kuwaelekeza wasomaji wake wao wote waje hapa kupiga kura hizo.. 

Utaweza kupiga kura moja katika kila kipengele (category) kila baada ya masaa 12. Ingawaje tutaruhusu watu waweze kushare kwa email zao maelezo ya kura hizi kwa watu mbalimbali ili watu hao waweze kushiriki lakini ufahamu kuwa tutazuia watu kwa kutumia cookies na Ip address. Tunajua njia zote zina mapungufu yake lakini tunaamini kuwa watu hawataenda extra miles ili tu waweze kupiga kura zaidi ya mara moja katika kipindi hicho cha masaa 12.

Tunajua tukitumia tu cookies watu wengine wanaweza kudelete, au kutumia browser tofauti na kupiga tena kura na tukizua Ip address tu wenye kutumia dial up, au proxy servers kama anonymous nayo unaweza kupiga kura tena. Hivyo kutokana na sababu hizo tumeamua kutumia njia zote mbili. 


Hivyo kama utaona huwezi kupiga kura yako kutoka kwa network au computer fulani basi ufahamu kuwa kuna mtu ametumia hiyo computer au network kupiga kura yake. Subiri kwa masaa kadhaa na ujaribu tena.

  
Nadhani tumeelewana lakini kama kuna mtu ana swali lolote basi usisite kutuandikia.

Tanzanian Blog Awards Team

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages