VODACOM FOUNDATION YATOA MSAADA WA MADAWATI SHULE YA MSINGI MSIGANI ILIYOPO MBEZI JIJINI DAR ES SALAAM - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

VODACOM FOUNDATION YATOA MSAADA WA MADAWATI SHULE YA MSINGI MSIGANI ILIYOPO MBEZI JIJINI DAR ES SALAAM


 Mwanafunzi wa shule ya msingi Msigani iliyopo mbezi jijini Dares Salaam, Answary Waziri  akisoma nembo kwenye moja ya dawati kati ya 50  yenye thamni ya zaidi ya shilingi milioni 4 yaliyotolewa msaada na Vodacom Foundation shuleni hapo.
 Baadhi ya wanafunzi wa shule msingi Msigani iliyopo mbezi jijini Dares Salaam, wakifurahia msaada wa madawati 50 waliyokalia  yenye thamni ya zaidi ya shilingi milioni 4 yaliyotolewa msaada na Vodacom Foundation shuleni hapo,shule hiyo ilikuwa inakabiliwa na uhaba wa madawati na madarasa.
 Baadhi ya wanafunzi wa shule msingi Msigani iliyopo mbezi jijini Dares Salaam, wakiangalia baadhi ya madawati  kati ya 50  yenye thamni ya zaidi ya shilingi milioni 4 yaliyotolewa msaada na Vodacom Foundation shuleni hapo.
 Meneja wa Vodacom Foundation Yessaya Mwakifulefule akiweka nembo kwenye moja ya dawati kati ya 50 aliyotoa msaada kwa niaba ya kampuni yake katika  shule ya msingi Msigani iliyopo mbezi jijini Dares Salaam, madawati hayo yana  thamani ya zaidi ya shilingi Milioni 4.
 Meneja wa Vodacom Foundation Yessaya Mwakifulefule akimsalimu mmoja wa wanafunzi wa  shule ya msingi Msigani iliyopo mbezi jijini Dares Salaam mara baada ya kufika shuleni hapo kutoa msaada wa madawati 50 yenye thamani ya zaidi ya shilingi Milioni 4,anaeangalia kushoto Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Zena Khakila.
Afisa Elimu  kata ya mbezi Veroni Mallya kushoto akishuhudia Meneja wa Vodacom Foundation Yessaya Mwakifulefula (kulia)akimkabidhi  Mwalimu Mkuu Zena Khakila wa  Shule ya Msingi Msigani iliyopo Mbezi jijini Dar es Salaam, msaada wa madawati 50 yenye thamani ya zaidi ya shilingi Milioni 4.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages