TBL YATOA MSAADA ZAHANATI BAGAMOYO - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

TBL YATOA MSAADA ZAHANATI BAGAMOYO


  Ofisa Uhusiano wa Kampuni ya bia Tanzania (TBL), Doris Malulu (kushoto) akimkabidhi Shujaa wa Safari Lager, Paul Luvinga jenereta na kompyuta iliyotolewa msaada kwa Jumuiya ya Maendeleo ya Wakazi wa Sinza E (JUMAWASE), kwa ajili ya maktaba ya eneo hilo. Pia katika hafla hiyo TBL  ilikabidhi msaada wa matofali 800 ya ujenzi wa Zahanati ya Kijiji cha Kidomole, wilayani Bagamoyo mwishoni mwa wiki. Wa pili kushoto ni Edward  Msigala Mjumbe wa JUMAWASE.
  Shujaa wa Safari Lager, Paul luvinga (kulia) akimkabidhi, Mwenyekiti wa Kijiji cha Kidomole, wilayani Bagamoyo, Mrisho Masoud, msaada wa matofali 800 yaliyotolewa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kwa ajili ya ujenzi wa Zahanati ya kijiji hicho. Hafla hiyo ilifanyika mwishoni mwa wiki katika kijijini hapo. Anayeshuhudia katikati ni Ofisa Uhusiano wa TBL, Doris Malulu.
Wakazi wa Kijiji Kidomole, wilayani Bagamoyo, Pwani, wakipanga matofali waliyopatiwa msaada na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), kupitia kwa Shujaa wa Safari Lager, Paul Luvinga kwa ajili ya ujenzi wa Zahanati ya Kijiji hicho. Hafla hiyo ilifanyika mwishoni mwa wiki kijijini hapo.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages